Usajili wa wachezaji wa ndani Simba hautoshi, waongeze wengine

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Leo nimemsikia semaji la CAF Ahmed Ally akielezea kuhusu usajili wa Simba, nimemsikiliza kwa umakini, amesema wamemaliza kusajili wachezaji wa ndani, ina maana Habib Kyombo na Nassoro Kapama ndio tumemaliza, waliobaki ni wa kimataifa ambao kiukweli bado watatu.

Mm naishauri timu yangu hii inayoninyima usingizi, timu niliyoanza kushabikia tangu kipindi kile marehemu John Makelele akimtungua marehemu Sahau Saidi Kambi, timu ninayoipenda kuliko zote duniani, CHONDE CHONDE, tuongeze wachezaji wa ndani, kwa sababu baadhi ya wachezaji wa msimu uliopita uwezo umepungua sana.

Jonas Mkude tayari ni maji ya jioni
Mzamiru Yassin pia maji ya jioni
Erasto Nyoni maji ya jioni
Tshabalala maji ya jioni
Kapombe maji ya jioni
Onyango maji ya usiku
Israel Mwenda maji ya jioni
Hassan Dilunga maji ya jioni
Kibu Dennis maji ya jioni

Naomba sana, Simba iwaongeze Salum Kihimbwa, Ismail Mhesa, kuna kiungo mmoja wa Ruvu mwili jumba halafu kuna kiungo mwingine wa Geita Gold alikuwa Ruvu anaitwa Naftar Nashon.Otherwise kuwategemea hao hapo juu tutakuja kulaumiana bure.
 
Hao wote sio maji jioni, hao ni sasa wameanza kula pensheni taratibu.
 
Yaani mpaka Israel Mwenda naye ni maji ya jioni!!
 
Acha kuzeesha watu wewe
 
Hao wote uliowatqjabkama wa jioni, wana ndoto ya kucheza Ulaya ukiacha Nyoni 😁
 
Safari wapinzani was jadi kila mmoja atakuwa na mghana tofauti zao mmoja anaitwa timu ya taifa hadi anagoma wakati meingine analalamika kwanini haitwi
 
Leo nimemsikia semaji la CAF Ahmed Ally akielezea kuhusu usajili wa Simba, nimemsikiliza kwa umakini, amesema wamemaliza kusajili wachezaji wa ndani, ina maana Habib Kyombo na Nassoro Kapama ndio tumemaliza, waliobaki ni wa kimataifa ambao kiukweli bado watatu.

Mm naishauri timu yangu hii inayoninyima usingizi, timu niliyoanza kushabikia tangu kipindi kile marehemu John Makelele akimtungua marehemu Sahau Saidi Kambi, timu ninayoipenda kuliko zote duniani, CHONDE CHONDE, tuongeze wachezaji wa ndani, kwa sababu baadhi ya wachezaji wa msimu uliopita uwezo umepungua sana.

Jonas Mkude tayari ni maji ya jioni
Mzamiru Yassin pia maji ya jioni
Erasto Nyoni maji ya jioni
Tshabalala maji ya jioni
Kapombe maji ya jioni
Onyango maji ya usiku
Israel Mwenda maji ya jioni
Hassan Dilunga maji ya jioni
Kibu Dennis maji ya jioni

Naomba sana, Simba iwaongeze Salum Kihimbwa, Ismail Mhesa, kuna kiungo mmoja wa Ruvu mwili jumba halafu kuna kiungo mwingine wa Geita Gold alikuwa Ruvu anaitwa Naftar Nashon.Otherwise kuwategemea hao hapo juu tutakuja kulaumiana bure.
Kama kweli alichosema msemaji wa Simba kuhusu kufunga usajili wa wachezaji wa ndani itabaki hivyo hivyo basi mashabiki wa Simba wajiandae na maumivu tena msimu huu. Simba itashiriki mashindano mengi mwakani hivyo basi ilitakiwa pia isajili wachezaji wa ndani wenye uwezo mkubwa. Wachezaji wa ndani nao ni muhimu sana hasa kwa mechi za mikoani kwenye viwanja vibovu kama lile shamba la mpunga kule Manungu ambapo wachezaji wengi wageni huwa wanapata shida. Nilitegemea Simba kwenye dirisha hili wafanye yafuatayo kuhusiana na wachezaji wa ndani :-

1. Kapombe alitakiwa atafutiwe msaidizi mwenye uwezo. Hapa ndio mpaka leo sielewi ni nani alitoa maamuzi ya kumuacha Duchu halafu akaletwa Mwenda kisa tu alifunga goli la faulu akiwa na Taifa Stars. Ikitokea kwa bahati mbaya Kapombe akapata majeraha yatakayomuweka nje kwa muda mrefu nafikiri hapo Simba ndio watajua kosa walilolifanya kwenye dirisha hili la usajili kuhusiana na mbavu ya kulia.
2. Mohamed Hussein naye alitakiwa apatiwe msaidizi mweye uwezo kama wake wa kuipandisha timu kushambulia. Gadiel Michael kweli anakaba vizuri sana lakini ni mzito wa kupandisha mashambulizi na hata akipanda hana uwezo wa kupiga krosi zenye macho na muda mwingi wa mchezo yeye ni kupiga "back pass" tu. Kwa akili zangu mbovu ningekuwa kwenye kamati ya usajili Simba ningeeda kuwaomba Azam hata kwa mkopo yule Edward Manyama ambao wao Azam wameshindwa jinsi ya kumtumia huyo beki wa kushoto.
3. Eneo la beki wa kati Kennedy bado anahitajia kwani kila akipewa nafasi anaonyesha bado ana uwezo licha ya mapungufu yake madogo madogo.
4. Eneo la kiungo mkabaji lilihitajika mtu kweli kweli wa kugongana hasa pale kati kati mwenye uwezo wa kuilinda "back four" zake kwa dakika zote tisini. Sitaki kusema lolote kwa sababu ni mapema sana labda kiraka Kapama anaweza kuja kuifanya hiyo kazi vizuri. Eneo hili kumtegemea Mkude ni maumivu kwani Mkude anakuwa mzuri tu akiwa na mpira miguuni kwake. Mpira ukiwa miguuni kwa adui Mkude hana ujanja wowote. Pia Mkude hana kasi uwanjani. Muzamiru naye akicheza kiungo mkabaji ni tatizo kwa sababu yeye ni aina ya viungo ambao hawawezi kukaa nyuma muda wote wa mchezo kulinda mabeki wake kwani mara nyingi utamkuta kwenye "box" la timu pinzani anashambulia. Pamoja na Simba kumsajili Akpan walitakiwa pia wasajili mchezaji mwingine mgumu wa ndani kwenye eneo hili.
5. Eneo la kiungo mshambuliaji nilitegemea Simba wamsajili kiungo mtundu mtundu mwenye kasi na ubunifu ili kumpunguzia kazi Muzamiru. Hapa nilitegemea kumuona Mkandala kwenye jezi ya Simba wala sio ya Azam anayokwenda kuivaa.
6. Kwenye ushambuliaji ni wapongeze kwa kumsajili Habibu Kyombo ila sitegemei kumuona Yusuph Mhilu akiendelea tena kuivaa jezi ya Simba kwani imekuwa kubwa sana kwake. Dilunga asiachwe asubiriwe kwanza apone majeraha yake ili afanyiwe tathmini kama majeruhi yameharibu kiwango chake au bado wa moto. Mwanuke aachwe aendelee kukua kwani ameonyesha ana kipaji na umri wake bado mdogo kwa hiyo ni hazina kwa siku zijazo na ndio vilabu vingi duniani hutumia mfumo huo kupata wachezaji wazuri wa baadae.

Narudia tena mtizamo wangu hapo juu ni kwa wachezaji wa ndani wa Simba sitaki kuzungumzia wachezaji wa kigeni kwa sababu usajili wao bado haujakamilika.

Ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom