Usajili wa wachezaji wa Simba ulivyotikisa na matokeo ya sasa

pilau

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
1,595
Reaction score
451
Yaani hakuna ubishi kila mpenda soka Tanzania alipoona hekaheka za usajili Kwa akili ya klabu ya Simba alikubali kwamba Simba wameamua na mambo yatakuwa safi

Lakini pamoja na gharama MO alizoingia za kunyang'anya wachezaji waliokuwa katika uwezo kutoka timu za ligi ya Tanzania kama salamba, kaheza, Mohammed kutoka prison na wengine kibao.

Na usajili wa akina wawa, nyoni, kappmbe na wengine wengi tena Kwa gharama na mishahara wachezaji wanayopata ni dhahiri kwamba matokeo hayaendani na thamani ya wachezaji waliopo licha ya kupoteza mechi kimataifa lakini hata wanapokutana na timu za hapa Tanzania performance ni mbovu na uwezo wa wachezaji baadhi ni wa kutiliwa mashaka. Nani anayewatafutia Simba Hawa wachezaji ?

Utashabgaa timu I na wachezaji wa kimataifa Rwanda, Ivory coast, Zambia, Uganda, Ghana nakadhalika lakini wakikutana na wachezaji wa bongo ni aibu tupu.

Ni wakati sasa umefika wa Simba kuwa na mkakati wa kuwa na usajili wa kisasa kuliko kuletewa wachezaji kwenye gunia na hawana msaada wowote kitaifa na kimataifa.

Haiingii akili ni kufungwa kizembe tena magoli mengi Kwa timu inayojiita bora kuliko zote Tanzania
 
Wachezaji hao baada ya miaka zaidi ya 10 ndio wamefanikisha kuipeleka simba makundi klabu bingwa Africa , kuwa na adabu na jasho la watu
Inaonyesha jinsi ulivyo mbumbumbu katika ufafanuzi ... Tumia ubongo usitumie kinyesi chako kilichobaki wakati unatawadha .... Kwani nani hana adabu Kwa jasho la watu... ? Nazungumzia usajili wa kitapeli unaofanywa Kwa vilabu na watu wabovu angalia usiwe miongoni
 
Wachezaji hao baada ya miaka zaidi ya 10 ndio wamefanikisha kuipeleka simba makundi klabu bingwa Africa , kuwa na adabu na jasho la watu
Inaonyesha jinsi ulivyo mbumbumbu katika ufafanuzi ... Tumia ubongo wakati wa kujibu hoja usitumie kinyesi chako kilichobaki wakati unatawadha .... Kwani nani hana adabu Kwa jasho la watu... ? Naxungumzia usajili wa kitapeli unaofanywa Kwa vilabu na watu wabovu angalia usiwe miongoni
 
Utapeli upi wacha bange wewe , utapeli unaweza kumpeleka mtu kwenye klabu 16 bora Africa ? hivi wewe unajua soka kweli ? usajili wa simba ni mzuri kuliko team yeyote Africa mashariki na kati, ndio maana ndio team pekee iliopo 16 bora Africa kutoka ukanda huu wote wa Africa mashariki na kati ,kufungwa mechi mbili kelele tupu , ebu wacha kelele
 
Kabisa na ndio timu inayoongoza sasa kugongwa magoli 10 ktk mechi 2 mfululizo za ligi husika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuingia 16 Bora sio sababu ..mlicheza na Nkana ambao sio mabingwa Zambia..miaka 17 wamechukua kombe la kwao mara moja...Is Soura sio mabingwa kwao..ndio maana ukikutana na mabingwa unakula kiganja.. hata Taifa Al Ahly anakupiga..Kama uliona Jana wakaacha kufunguka ili Simba acheze Waone strengh yao..wanafanyia kazi..
Alafu wachezaji 9 Bora hawakuwepo...tafsiri ya kikosi kipana
 
Sasa kikosi cha simba unakipima kwenye nini kama sio mafanikio, na katika level ya vilabu Africa klabu bingwa ndio mafanikio ya juu, Simba amepenya ameingia 16 bora halafu unakuja hapa unabeza mafanikio ambayo toka 2005 hakuna aliethubutu kufika huko , hivi unajua soka kweli wewe? kiufupi Simba amesajili kwa bilioni tumeingia 16 bora tumepata Bilioni yaani Pesa ya usajili imerudi halafu unapinga mafanikio hayo huo ni ugonjwa wako
 
Kabisa na ndio timu inayoongoza sasa kugongwa magoli 10 ktk mechi 2 mfululizo za ligi husika

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna tabu hatua aliofika anastahili pongezi zaidi ni team mbili tu Tanzania 1998(yanga mpaka leo ajarudi) , Simba mara mbili tu ikiwepo hii 2018 , hivyo amefanya jambo kubwa kama kufungwa ata Madrid alifungwa 5 na Barcelona
 
Sawa Simba wameingia 16 bora tunawapongeza lakini kukosolewa kupo pale pale magoli 10 kwa mechi mbili si jambo la kitoto lazima ukweli ubaki kuwa ukweli kwamba kwa soka letu hili la kisiasa tutaendelea kutia aibu,wenzetu wamewekeza sana kwenye soka sisi tumewekeza kwenye porojo,wapi na wapi?
 
ushabiki wa Simba toka mwanzo ulikuwa na matatizo kama wawa alianzxa kulalamikiwa toka anakuja lakini viongozi wakaziba macho wakamsajili wengi walisema ni mzito lakini kwa sababu tulikuwa tunacheza na timu za kawaida makosa yake hayakuonekana, gyan naye ni tatizo kubwakwanza hakusajiliwa kucheza beki alisajiliwa kucheza mshambuliaji matokeo yake baada ya kuumia kina Nyoni na Kapombe tunakosa mbadala tunabaki kulaumu kipa nan makocha hata Simba hawana mbadala wa Manula kwani kiwango cha dida bado kipo chini halafu viongozi wanashindwa kuwa na malengo wanakubali simba itumike kisiasa kwa kushiriki makombe kama mapinduzi ambayo hayawapeleki popote zaidi ya kuwapatia majeruhi kamailivyotokea kwa Nyoni
 
Timu ni nzuri tatizo liko kwa wachezaji na makocha nahisi kuna mdudu ameingia pale msimbazi mdudu kama huyu aliingia pale man utd akasabisha kocha kufukuzwa kisa matokeo mabaya waleta Olegna ambaye profile yake inaonyesha ni mchezaji mwenye mafanikio lakini nikocha aliyeshusha timu daraja Katua Utd anapata matokeo ya kuishangaza dunia kwahiyo hapa huenda wachezaji wa simba wamezidisha ngono sababu ya vihela wanavyopewa mitaani na mashabiki au kocha ameishiwa mbinu hata mashabiki nao nitatizo kunakitu wameingiziwa akilini mwao eti simba ina kikosi kipana sio kikosi ni midomo mipana nahii midomo yaondio inawacost

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpira unahitaji Muda na malengo ya muda mrefu huwezi kupata mafanikio ya haraka hivyo simba tumeanza hatukati tamaa kipigo ni kawaida ktk Mpira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii si lugha ya kiungwana katika mijadala tuvumiliane madhaifu yetu lakini ikiwa wengine tuko smart zaidi ya wengine basi tuoneshe u smart katika kuwa Msaada kwao wasiojua unamtolea mwingine maneno ya hovyo ambayo pia yanakurudia wewe mwenyewe, ndugu rekebisha tabia yako ifae kuitwa MTU na Utu.

Sent from my TA-1021 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…