Usajili wa Yanga kila mwaka hauridhishi kiu ya washabiki, kulikoni?

Usajili wa Yanga kila mwaka hauridhishi kiu ya washabiki, kulikoni?

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Posts
2,180
Reaction score
1,291
Bila kuficha usajili wa yanga una kasoro kubwa sana kila mwaka. Hivi ni kwa nini yanga hupenda kusajili asilimia kubwa mitumba mikubwa kutoka nje ya nchi na kudharau wachezaji wenyeji? Hii dhana ya kufikiria eti ukijaza wageni wengi ndani ya timu kuna manufaa kuliko kusajili wachezaji wetu wa ndani, hukera sana.

Leo tena Yanga ina msaka Heltier Makambo badala ya kuwinda mfungaji wa JKT Ruvu! Mchezaji wa nje ambaye klabu yake imemtoa kwa mkopo na halafu huko alikwenda kwa mkopo hapangwi utaona yanga inamnunua kwa bei mbaya! Huku ni kuleta maudhi na matumizi mabaya ya bajeti ya usajili.

Ukweli ni kuwa a graet man does not born great but grow great una maana wachezaji wetu wa ndani wenye vipaji wanweza kuja kuwa tishio duniani ikiwa makocha wetu watawaendeleza na kuwapa fursa ya kujifunza zaidi mbinu za mpira. Yupo wapi yusufu mhilu, Adam salamba na maheza? wote hawa wamepondwa kwa sababu ya kuzoa wachezaji wanao kushuka kipawa tu. Je, wale waliopanda daraja kutoka timu B wameishia wapi?

Yanga thamini vipaji vinavyokuwa kuliko kubeba mizigo ambayo huishia kutemwa hovyo.
 
Hawawezi kumsajili kwasababu wewe umesema!

Kuna bench la ufundi wana mipango yao pia
 
Naona unachanganya mambo.

Adam salamba na kaheza washawahi kucheza Yanga?
 
Lugha ya Kiswahili inatosha sana kuwasilisha hoja.
 
Back
Top Bottom