Usajiri wa Samatta Paok. Mashabiki waonekana kutofurahia usajili wake

Usajiri wa Samatta Paok. Mashabiki waonekana kutofurahia usajili wake

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Club ya PAOK ya Nchini Ugiriki imetangaza Kumsajiri Mtanzania Mwenzetu SAMATTA akitokea Fenabache, Cha Kushangaza nimepia Comment za Mashabiki asilimia 99% hawajapenda Usajiri wake.

Kwa msaada wa Insta Translator nimeweza kuelewa wanacho kimaanisha, Wengi wanasema ni Striker Mbovu kuwahi Kutokea na Wanaionea Huruma PAOK, Katika Comment 1000+ za Tangazo la Kwanza La Samatta Kusajiriwa, Mashabiki wameoneshwa Kuchukizwa na Usajiri huo, Hawa Wagiriki wanataka kutwambia nini watanzania?

IMG_8634.jpg

IMG_8635.jpg

So hawa Wagiriki wanataka Kutwambia nini kuhusu Captain wetu?
 
UTO wachezaji wao wanaishia kuendesha Bodaboda[emoji2089][emoji2089][emoji2089]
 
Ukisikia kismati ndiyo hiki sasa. Kiukweli Kijana hana maajabu kwa sasa. Bora hata aengeendelea tu kubakia Genk.

Huko alikoenda, akiendeleza ile tabia yake ya uvivu, na hivyo kutumia muda mwingi kudhurura tu uwanjani, na kutoa vipasi vya hapa na pale; aisee msimu ukiisha tu atafungashiwa tena vilago.
 
Juzi nilikuwa naangalia vijana walioenda kuomba fursa Simba, aisee kusema kweli vijana wetu wana misingi mibovu sana ya soka. Imagine umri ule tayari unaona hawa madogo washapotea. Wakishafika umri wa kina Kyombo na Mzize tunawalaumu ila ni kama tunawaonea tu. Tuna misingi mibovuuu.
 
Soka lina Njia zake... BOOM... CRISIS... DEPRESSION... RECOVERY... ameshapitia zote... acha amalize soka lake...
 
Angekuwa Msuva angalau ila Samata dah hiyo kazi ni anamchomesha wakala nadhani hata ye amejitahidi ila wakati si wake
Kuna siku aliwahi kusema kama angepata nafasi ya kuomba kitu basi angeomba awe na umri mdogo wakati anaenda Europe
Si unaona kina Bailey na Ndid au Trosard hao wote walikuwa dream team ya Genk
 
Marcelo wa Madrid alifukuzwa aliposajiliwa Ugiriki kwa kuambiwa kiwango chake ni kidogo.
 
Ukisikia kismati ndiyo hiki sasa. Kiukweli Kijana hana maajabu kwa sasa. Bora hata aengeendelea tu kubakia Genk.

Huko alikoenda, akiendeleza ile tabia yake ya uvivu, na hivyo kutumia muda mwingi kudhurura tu uwanjani, na kutoa vipasi vya hapa na pale; aisee msimu ukiisha tu atafungashiwa tena vilago.
Hapa ndipo mnapokoseaga, hii ndio tafsiri ya ukubwa na kujua.Wazungu sio wavuta bangi, acha aendelee kukichafua.
 
Back
Top Bottom