Usalama Kenya

Usalama Kenya

Wakuu hii issue ya shakaola, Kenya inamaanisha nini?

Je, usalama wa taifa ni mdogo Kenya?

Kweli, anakufa mtu mmoja hadi mtu wa mia moja sabini na tisa, usalama wa taifa haujui?

Kenya ni nchi yenye matobo matobo, mpaka naingiwa na wasiwasi kuwa jirani nao.
 
Usalama wa Kenya ni mdogo sana. Unaweza safiri kutoka tarime mpaka Mombasa ukafanya mambo yako,ukarudi na usiulizwe wala kizinguliwa njiani.
 
Pale hamna nchi pale, kila mtu anaingia ananyamba anavyopenda, halafu anaondoka zake. Wee watu zaidi ya 200 wanauliwa halafu vyombo vyao havioni wala kusikia.
Mimi naonelea kwa hili Kenya ipewe onyo kali na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hii hali unaweza kuitofautishaje na makaburi ya pamoja yanayapatatikana mashariki mwa Congo (Kivu). Hayo ni mauaji sawa na mauaji mengine yanayopatikana katika maeneo yenye mizozo/vita. Kenya imezembea sana kuacha raia wasio na hatia kuuawa kwa kiasi kile. Hii haingii akilini kabisa, nchi ambayo inatuma na vikosi kwenda kutunza amani kwenye maeneo ya vita, huku kwake kukiwa kunaungua. Unakimbia kwa bidii zote kwenda kuzima moto kwa jirani wakati huo huo kwako hali ikiwa ni tete. Huo ni upendo usiofaa kitu, wala kutumia akili.
 
Back
Top Bottom