Samedi Amba
JF-Expert Member
- Nov 13, 2018
- 227
- 178
Habari wanajamvi,
Natumaini wote tunaendelea vizuri.
Moja kwa moja kwenye mada...
Nimekuwa mdau wa kununua vitu mtandaoni kwa muda mrefu. Imenilazimu sana kumtuma mtu endapo nafanya biashara na "mgeni" nisiyemfahamu. Kwa mfano, mwaka jana nilinunua laptop kwa mdau mmoja Mwenge, DSM. Ilinibidi kumtuma rafiki yangu kukagua mashine, na kunipa jibu kabla sijafanya muamala.
Aliponihakikishia, nilituma pesa kwa namba ya jamaa (muuzaji). Mara simu ikawa haipatikani. Kiwewe hichooo! Sema nadhani mtandao ulicheza na baadaye akanihakikishia kuwa fedha alipata. Tukamaliza mchezo.
Huwa nawaza kwa sauti... Hivi haiwezi kufika siku kukawa na "mfumo kati", yaani mfumo unaoniruhusu kununua bidhaa kwa usalama?
Wanavyofanya alibaba:
1. unaenda mtandaoni,
2. unatafuta laptop inayouzwa,
3. unaweka fedha kwenye mfumo,
4. jamaa anatuma laptop
5. unahakikisha ndo yenyewe
6. "unaruhusu" fedha. Yaani inaingia kwenye account yake na anakuwa na uwezo wa kutoa.
Hofu yangu ni kwamba wafanyabiashara wengi ni watu wa "papo hapo". Nahisi huenda wasiwe na subira ya kusubiri uhakiki huu.
Hivi, tofauti na kumtuma unayemwamini, je kuna njia mbadala? Je, kuna kampuni wanaoweza kufanya ukaguzi wa mzigo kabla haujatumwa? Au tafanyaje kuongeza usalama wa biashara mtandaoni?