Usalama wa nyumba zilizozungushiwa nyaya za umeme za ulinzi au electric fence

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Nyumba zilizozungushiwa nyaya za umeme za ulinzi au electric fence zinaonyesha ziko salama sana maana zinadili na njia kuu ya wizi au ujambazi kufanyika.

Mara nyingi huduma hii inaambatana na uwepo wa cameras ili kuongeza zaidi ulinzi.

Umewahi kusikia uvamizi umefanyika katika nyumba zenye electric fence?

Je, ukiweka hizo nyaya za ulinzi za umeme bila kuweka cameras, wahalifu wanaweza kata hizo nyaya na kuingia ndani kirahisi?

Nauliza haya maswali kwa sababu nataka kuweka ulinzi wa aina hii katika eneo la heka moja bila kutegemea sana cameras ingawa zitakuwepo chache.
 
Nyaya zake ni ngumu kukata pia ukikata inapiga alarm kali.
Sio ukitaka kukata ukitembelewa na nyoka au jani gumu au matawi magumu ya mti yakigusa alarm inalia bwiii bwiii mtatafuta shida ilipo hata ikiwa saa 1 usiku bila hivyo muwapigie wenyewe waliounga waje kucheck shida nini na hapo lazima mkaizime maana majirani hawatolala kwa hio mikelele ya alarm
 
Hizo waya zikiwashwa zina umeme na umeme wake ni wa kutosha kukubabua vizuri tu, namaanisha jinsi zinavyoungwa umeme wake unajitegemea na mtambo wake unajitegemea sasa wewe jisogeze kwenye high voltage uone kitakacho kupata utababuka

Nyaya zake ni ngumu kukata pia ukikata inapiga alarm kali.
Vipi umeme ukiwa umekatika au zina mfumo wa dharura wa kuhifadhi umeme?
 
Hii si ndio walivyomfanyia yule mama kule mwanza ila waliwaua
Security ni multifaceted

Kuna

Deterrence - aone uvivu au shida au risk kuingia kwako, au ajaribu ila umcheleweshw ili aghairi - electric fence, mageti na milango iliyo secure, lighting. Waliokutarget hawazuiwi na haya.

Detection - Akiingia upate taarifa mapema kabla hajafika mbali - motion & presence detectors. Itakusaidia kama una silaha kuwawahi.
 
Kwa maoni yangu ulinzi madhubuti wa makazi unahitaji levels nne za ulinzi:
1. Electric fence
2. Cameras - ikiwezekana kuwe na mtu wa kuzimonita masaa 24 au kama haiwezekani basi zirekodi matukio yote na kuyahifadhi katika server iliyopo hapo nyumbani au online kwa muda fulani ili tukio lolote likitokea uwe na pa kuanzia.
3. Motion detectors au alarm system - hizi unaweka ndani hasa kwenye milango ya kutoka nje. Motion detectors unaweza pia kuweka sebuleni na jikoni mkienda kulala.
4. Mlinzi. Uwepo wa mtu utasaidia kucover mapungufu yoyote ya mifumo hiyo hapo juu na kuwa mtu wa kwanza kureact.
 
Vipi umeme ukiwa umekatika au zina mfumo wa dharura wa kuhifadhi umeme?
Mfumo wake ni separate kabisa na umeme wa nyumba ila umeme ni huuhuu kwenye kuunga ndio wanatenganisha ila kwa wenye pesa nyingi unaungwa na standby generator ile ya hapo kwa hapo isiyopiga makelele niliikuta sehemu moja tu umeme ukizima generator linawaka fasta hapo hapo na ukirudi linasubiri dakika kadhaa linajizima lenyewe huwezi jua km kuna generator maana halipigi kelele, nazungumzia wenye pesa
 
Kwa maoni yangu ulinzi madhubuti wa makazi unahitaji levels nne za ulinzi:
1. Electric fence
2. Cameras - ikiwezekana kuwe na mtu wa kuzimonita masaa 24 au kama haiwezekani basi zirekodi matukio yote na kuyahifadhi katika server iliyopo hapo nyumbani au online kwa muda fulani ili tukio lolote likitokea uwe na pa kuanzia.
3. Motion detectors au alarm system - hizi unaweka ndani hasa kwenye milango ya kutoka nje. Motion detectors unaweza pia kuweka sebuleni na jikoni mkienda kulala.
4. Mlinzi. Uwepo wa mtu utasaidia kucover mapungufu yoyote ya mifumo hiyo hapo juu na kuwa mtu wa kwanza kureact.
Mkuu hao wote kiongozi wa kwanza ni mbwa.

Mbwa aliyefunzwa ni hatari.
 
Mfumo wake ni separate kabisa na umeme wa nyumba ila umeme ni huuhuu kwenye kuunga ndio wanatenganisha ila kwa wenye pesa nyingi unaungwa na standby generator ile ya hapo kwa hapo isiyopiga makelele niliikuta sehemu moja tu umeme ukizima generator linawaka fasta hapo hapo na ukirudi linasubiri dakika kadhaa linajizima lenyewe huwezi jua km kuna generator maana halipigi kelele, nazungumzia wenye pesa

Ina betri inakaa masaa manne.
Kwa uhakika zaidi hapo automatic generator muhimu au ziendeshwe na solar power.
 
Kwa maoni yangu ulinzi madhubuti wa makazi unahitaji levels nne za ulinzi:
1. Electric fence
2. Cameras - ikiwezekana kuwe na mtu wa kuzimonita masaa 24 au kama haiwezekani basi zirekodi matukio yote na kuyahifadhi katika server iliyopo hapo nyumbani au online kwa muda fulani ili tukio lolote likitokea uwe na pa kuanzia.
3. Motion detectors au alarm system - hizi unaweka ndani hasa kwenye milango ya kutoka nje. Motion detectors unaweza pia kuweka sebuleni na jikoni mkienda kulala.
4. Mlinzi. Uwepo wa mtu utasaidia kucover mapungufu yoyote ya mifumo hiyo hapo juu na kuwa mtu wa kwanza kureact.
Hio 1 mpaka 3 ni kitu kimoja huo ni mfumo na hio namba 4 ni inakua hapo kusimama nyuma ya mfumo kikitokea chochote kimefanyika na kugunduliwa na mfumo basi namba 4 anachukua hatua ya kukagua na kuchukua hatua na wengi hufanya hivyo, upo sahihi kabisa mkuu hio ipo sehemu nyingi nyingi nyingi hakuna penye camera pasiwe na mtu wa kukagua kufanya uangalizi km kuna kajizi kananyemelea maeneo
 
Mfumo wake ni separate kabisa na umeme wa nyumba ila umeme ni huuhuu kwenye kuunga ndio wanatenganisha ila kwa wenye pesa nyingi unaungwa na standby generator ile ya hapo kwa hapo isiyopiga makelele niliikuta sehemu moja tu umeme ukizima generator linawaka fasta hapo hapo na ukirudi linasubiri dakika kadhaa linajizima lenyewe huwezi jua km kuna generator maana halipigi kelele, nazungumzia wenye pesa
Mkuu,
Kwa manufaa ya jukwaa. Umeme unaotumika ni wa majumbani. Tofauti umeme wake ni DC yani direct current na umeme wa majumbani ni AC yani alternate current.

Kinachofanyika ni kuwa controller yake ina AC to DC converter ambayo ubadili umeme wa kawaida AC kuwa wa DC.

Uwepo wa DC power ndio inafanya zile nyaya kuwa hatari zaidi.

Pia controller yake ina inbuilt betri inayokaa masaa manne iwapo umeme ukikatika.

No need of backup generator...
 
Back
Top Bottom