Heshima mbele wana Jamvi wenzangu..... Nimesoma hii kitu hapa chini kwenye Nipashe la leo kwa kweli imenishtua kidogo..... Kwa ufahamu wangu ni kwamba wengi wetu tutasema hii ni "Isolated incidence" lakini je, tuiachie hapo?? Watoto wetu mashuleni watakuwa salama?
Mwanafunzi awashambulia wenzake kwa kisu darasani
2008-10-29 12:32:58
Na Boniface Luhanga
Wanafunzi wanne pamoja na mwalimu wao wa Shule ya Sekondari St. Peter`s iliyoko Kimara, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wamejeruhiwa vibaya baada ya mwanafunzi mmoja wa shule hiyo kuibuka ghafla darasani na kuwashambulia kwa kisu.
Tukio hilo la kusikitisha, lilitokea jana saa 2:45 asubuhi baada ya mwanafunzi huyo, Aaron Mbando, anayesoma kidato cha tatu shuleni hapo, kuinuka ghafla darasani na kuchomoa kisu mfukoni mwake na kuanza kuwachoma visu wanafunzi wenzake pamoja na mwalimu wao aliyekuwa akifundisha somo la Jiografia kwa wakati huo.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Leticia James, aliwataja wanafunzi waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Eva Daza, Siwatu Abdallah, Esther Soter, Anzuruni Anzuruni pamoja na mwalimu Peter Salema.
Mwalimu James alifafanua kuwa, wanafunzi Eva na Siwatu, walijeruhiwa vibaya kichwani, mgongoni, miguuni na mikononi.
Alisema majeruhi hao wote wa kidato cha tatu, walipelekwa katika zahanati ya serikali ya Kimara na kupewa huduma ya kwanza ikiwemo kushonwa nyuzi kadhaa kwenye majeraha ambapo Eva na Siwatu, baadaye walikimbizwa hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kimara, Dk. Regina Elias, alithibitisha kuwapokea majeruhi hao na kueleza kwamba, wawili kati yao walipata majeraha makubwa.
``Wawili kati yao, wamepata majeraha makubwa ambapo mmoja amechomwa kisu kichwani na kimezama sana na kusababisha atokwe damu nyingi...kwa zahanati hii, hatuwezi kudhibiti hali hiyo na ndiyo maana tumeshauri pamoja na mwenzake, wapelekwe Mwananyamala kwa matibabu zaidi,`` alifafanua.
Nipashe ilishuhudia gari dogo lenye namba za usajili T 148 AJA likiwabeba majeruhi hao kuwapeleka hospitali ya Mwananyamala.
Akisimulia mkasa huo, mwanafunzi aliyenusurika kujeruhiwa, Mary Patrick wa kidato cha tatu, alisema wakiwa darasani wakifundishwa somo la Jiografia na mwalimu Salema, ghafla mwanafunzi mwenzao Aaron, alisimama na kumchoma kisu Eva aliyekuwa ameketi karibu naye.
Alisema tukio hilo liliwashtua wanafunzi wote ambapo mwalimu wao, Salema alijaribu kumfuata kwa lengo la kumdhibiti, lakini naye pia alichomwa kisu kichwani.
``Ndipo wanafunzi wote pamoja na mwalimu, tukaanza kusukumana mlangoni kila mmoja akijaribu kukimbia kuokoa maisha yake,`` alisema.
Alisema wakati wakisukumana mlangoni, ndipo mwanafunzi huyo Aaron, alipopata nafasi kuwachoma visu kila mwanafunzi aliyefanikiwa kumfikia.
``Kulikuwa na kelele zisizokuwa za kawaida, hali iliyowashtua walimu na wanafunzi waliokuwa kwenye madarasa mengine ambao walifika eneo la tukio kutaka kufahamu kulikoni,`` alifafanua.
Alisema hadi wanafanikiwa kutoka nje ya darasa, mwanafunzi huyo alikuwa tayari amewajeruhi wanafunzi wanne pamoja na mwalimu.
Hata hivyo, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Leticia James, alisema wiki kadhaa zilizopita, mwanafunzi huyo aliyewajeruhi wenzake, hakuhudhuria shuleni.
Alisema baadaye, alirejea shuleni ambapo mzazi wake alidai kwamba, mtoto wake alikuwa ametoweka nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha.
Mwalimu Mkuu Msaidizi huyo aliongeza kuwa, mzazi wa mwanafunzi huyo pia alidai kuwa, mtoto wake alikuwa akikabiliwa na matatizo ya akili.
Hata hivyo, alisema tangu aliporejea shuleni hapo takriban wiki moja, hakuonyesha dalili zozote za kuumwa hadi jana alipofanya kitendo hicho.
James alisema uongozi wa shule, haukuweza kufahamu mara moja namna mwanafunzi huyo alivyoweza kuingia na kisu darasani na kwamba kwa kawaida, hawana utaratibu wa kuwakagua wanafunzi mifukoni mwao kama wanaingia madarasani na vitu vya hatari zikiwemo silaha.
Mwanafunzi aliyefanya unyama huo, pia alijeruhiwa vibaya kichwani na ilidaiwa kwamba alijichoma mwenyewe kwa kisu baada ya kuwajeruhi wenzake.
Hata hivyo, mwanafunzi huyo alikamatwa na kufikishwa kituo Kidogo cha Polisi Kimara na baadaye kuchukuliwa kwa gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili PT 1412 na kupelekwa kituo cha Polisi Magomeni.
Ilidaiwa kuwa, ilikuwa ni kazi kubwa hadi kufanikiwa kumkamata mwanafunzi huyo kutokana na kuwa na kisu mkononi.
Na alipohifadhiwa katika kituo kidogo cha polisi Kimara, mwanafunzi huyo alisikika akipiga kelele huku akigonga gonga mlango kwa nguvu akitaka afunguliwe atoke.
Hili ni tukio la pili linalofanana na hilo la jana kutokea ambapo zaidi ya mwezi mmoja uliopita, mgonjwa mmoja wa akili, aliwashambulia wagonjwa wenzake katika wodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuwaua wawili huku wengine watano wakijeruhiwa vibaya.
SOURCE: Nipashe