Usalama wa Taifa uboreshwe...

Usalama wa Taifa uboreshwe...

simon mato

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2015
Posts
926
Reaction score
485
Ndugu wanajamvi,

Kwa kuwa kazi ya TISS ndiyo kazi ambayo Mimi navutiwa nayo sanaa katika maisha mathalani ukiachilia shughuli zangu za hapa na pale ata itikadi zangu kisiasa. Ni maoni yangu kuwa hii idara nyeti ingeboreshwa katika mfumo wake.

Tiss ingejigawa kwenye makundi mawili kama ifuatavyo;

1: kundi la kwanza lishugulike na mambo ya nje ya nchi; hawa wafanye kazi kubwa kuspy mataifa makubwa kinagaubaga ikiwezekana iajiri hadi maafisi wake nje ya nchi kwa ajili ya kupanua mtandao wao wenye wigo mpana kama CIA .

Ni vyema ili lifanyike kwa kuwa itatusaidia kupata siri nyingi za nchi zingine kwa kuwa sote tunajua nchi za wenzetu walivoendelea kwenye hii idara.

2: kundi litaloshughulikia mambo ya ndani: hawa ndo wangekuwa kama FBI hii ingesaidia sanaa kuwajengea uwezo wa kufahamu nchi yetu vizuri. Wafanye kazi zao kiuledi ndani ya nje ya nchi.

Mwisho ningeomba mkurugenzi wa TISS angeangalia vijana wazalendo na wanaonekana wenye uwezo huu kutokana na historia au ufahamu wao kama " The Bold " na wengine wangeitwa na kuhojiwa kama wangeweza kusaidia hii kazi ili wapewe mafunzo maalum ili wajiunge kusaidia hili taifa kwa sababu inaonekana wana vitu vya ziada.


FBI au CIA wana mtandao mpana sanaa kuna hadi majambazi walioshindikana wenye vitu vya ziada na wafungwa wa
jela wenye vitu vya ziada hupewa mafunzo maalum kujiunga na hivi mashirika.Ni vyema wajiimarishe kila secta na wawe na vijana wazalendo na taifa hili.
 
Back
Top Bottom