Kama kuna idara ya serikali inatakiwa kuwajibika kwa uhalifu dhidi ya wananchi ni hii ya usalaama wa Taifa ambayo kutokana na utendaji kizembe nchi imepata hasara kubwa kabisa. Hapa kuna moja kati ya facts hizi mbili:
Ya kwanza ni labda hawaelewi kwamba wajibu wao si kumlinda Rais na viongozi wa serikali tu bali kulinda hujuma dhidi ya taifa kama zile za kufuru ya wizi uliofanyika Benki Kuu wa EPA, Benki Kuu ndiyo kidundio (Apex) cha moyo wa taifa lolote ambapo hujuma yoyote dhidi yake ni sawa na angamizo la uchumi. Zipo pia hujuma za Mikataba ya rushwa, Richmond, Meremeta, Kiwira n.k. zimetendeka wakiwa busy "kuwalinda " wahujumu hawa wa uchumi wetu ambao kwa kweli ndiyo maadui wa kweli wa nchi yetu. Na sasa ndiyo tunapata kichefuchefu kabisa kusikia wamehusika na vote rigging zinazolenga kuharibu utashi wa wananchi!
Pili ni kwamba huenda wanadhani wanapaswa kuwajibika kwa viongozi wanaowateua, lakini sijui kama wanajishughulisha kuelewa mishahara wanayolipwa inagharimiwa na nani.
Usalama wa taifa wa kwetu wanafanya kazi ki-primitive kwelikweli, hebu angalia; wenzetu kule Marekani walikuwa usalama wa Taifa wao waliogundua hila alizotumia Rais Nixon kushinda uchaguzi walimpeleleza, wakawakabidhi Polisi ambao waliwasilisha tuhuma Bungeni ambapo baada ya kuzithibitisha wengi walichukuliwa hatua na Rais kulazimishwa kuachia ngazi. Mambo ni hivyohivyo kule Uingereza ambako kina Chenge waligunduliwa kugawana rushwa ya ununuzi wa Rada na Ndege. Hapa hakuna cha Usalama wa Taifa wala kitengo cha upelelezi chenye ubavu wa kufanya hivyo, labda ni kwa sababu ya kulipwa fadhila ya kupewa ulaji na Rais ambaye anayo pia madaraka ya kuwaondoa hata kwa kuwaonyeshea kidole tu.
Kwa mtaji huu Usalama wa taifa wataendelea kuwa mzigo wa taifa na aibu kubwa kwa nchi yetu.