Usalama wa Taifa

Usalama wa Taifa

Kinjekitile junior

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2015
Posts
4,404
Reaction score
581
Tanzania imekuwa nchi ya kupigiwa mfano ndani na nje ya Bara la Afrika kwa kuwa na Amani na Utulivu uliotukuka kutokana na uthabiti wa Ulinzi na Usalama.Kwenye Katiba Inayopendekezwa ile Ibara ya 265 kuanzia kifungu cha (1) kinaeleza kuwa jukumu la Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano ni la kila raia.

(2) Usalama wa Jamhuri ya Muungano unahusu ulinzi wa mipaka yote ya eneo la Jamhuri ya Muungano kama ilivyoainishwa katika ibara ya 2 ikiwa ni pamoja na ardhi ,anga ,mito,maziwa, visiwa na bahari kuu watu wake, mali zao haki ,uhuru na maslahi mengine ya kitaifa dhidi ya vitisho vya ndani na nje ya nchi.

Ibara ya 266 Inavitaja vyombo vya ulinzi na usalama
a.JWTZ
b.Jeshi la Polisil la Jamhuri ya MUUNGANO na
c.Usalama wa Taifa.

Msingi mzuri uliopo na unaotajwa katika Katiba Inayopendekezwa kwa kutambua nafasi ya raia katika jukumu la Ulinzi na usalama unapaswa kuungwa mkono na kila mpenda Amani na Utulivu. Mungu Ibariki Tanzania.

Nawasilisha.
 
Mimi sijaelewa hoja yako, naona umenukuu tu vifungu vya Katiba na kuvibandika vizimavizima bila kuweka hitimisho lako.

Vv
 
Kweli Tz inaendelea kusonga mbele,kikubwa wananchi tuendelee kuunga mkono hali iliyotufikisha hapa,kila mmoja wetu awe mlinzinwa taifa letu!!
 
Kwani amani kuwepo ni kwa sababu ya Katiba pendekezwa? Jipange upya!
 
Kwani amani kuwepo ni kwa sababu ya Katiba pendekezwa? Jipange upya!

Ninachokiona hapa ni kuelewa content, mtoa mada kaonyesha msimamo wake kwa kusema Amani na utulivu uliopo umejengwa,na msingi wake mkuu umesababishwa na ushiriki wa raia wote katika jukumu la ulinzi na usalama wa nchi yao!!!
Katiba inayopendekezwa ukisoma ibara alizotaja zinapita mulemule kuhakikisha kuwa taifa letu linaendelea kuimarika kwa kuwa na amani na utulivu kwa kuweka wazi jukumu hilo kwa raia wote!!!
 
Mimi sijaelewa hoja yako, naona umenukuu tu vifungu vya Katiba na kuvibandika vizimavizima bila kuweka hitimisho lako.

Vv
Hata kama kabandika vifungu, kwani hapa tuko kwenye ushindani wa kujua kuweka hoja ama kuelimishana? Tumiaga akili sometimes kijana!
 
Tanzania itajengwa na wenye moyo na siyo wenye maneno matupu. Maneno maneno hayatupelekipopote zaidi ya kupigiwa makofi, turn those words into actions.
 
Back
Top Bottom