Usalama wa vyakula kukaa muda mrefu kwenye Friji

Mwalaye

Senior Member
Joined
Jun 17, 2021
Posts
171
Reaction score
233
Niko single. Mwanzoni mwa mwezi huwa nachemsha kilo mbili za maharage. Yakisha poa nayaweka kwenye Friji.
Sasa huwa nachota kidogo nakaanga, nasonga ugali, siku imepita.
Kwa mtimdo huu harage hilo huwa linadumu mwezi mzima.
Je, wadau hii ni salama kwa afya?
 
Mkuu hongera saana...unakula maharage kilo 2 kwa mwezi.

Binafsi chakula kikaa zaidi ya siku mbili kwa fridge huwa napata shida ya tumbo.

Kwenye freezer sawa.
 
Mkuu naamini huwa yanafanya yanakuwa kama jiwe! Hapo wewe endelea kutwanga harage mkuu wasikutishe!
 
Kama haikuletei shida we endelea mkuu, huwezi chemsha maharage kila siku kama ni mpenzi wa maharage
 
Kwa kuwa tulio wengi tunakula ili kujaza tumbo nadhani haina shida
 
hayo ya kukaa mwezi kwenye friji siyanakuwa magumu kama jiwe kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…