Usalama wa wageni waimarishwa Zanzibar, je ni chanzo cha ongezeko la watalii?

Usalama wa wageni waimarishwa Zanzibar, je ni chanzo cha ongezeko la watalii?

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Naibu Waziri,Ofisi ya Waziri mkuu kazi,vijana,na ajira pia mbunge wa chama cha mapinduzi jimbo la Shinyanga mjini Mh Paschal Katambi ametembelea katika uwanja wa ndege wa Shekh Abeid Amani Karume Zanzibar kwaajili ya ukaguzi wa mifumo ya usalama na utoaji huduma kwa wageni wanaoingia nchini na watanzania wanao tumia uwanja huo.

Paschal amesema pia kuangalia usalama wa raia na wageni wanao kuja nchini, wakiwa wametoka maeneo mbalimbali, na kuona pia huduma ambazo wanazozipata na urahisi wa huduma kulingana na maelekezo ya Mheshimiwa Rais ya kuweka mifumo ya Kidijitali.

Soma zaidi :Nikilio na kusaga meno,Hakuna watalii kabisa Zanzibar

Amesema wameweza kutekeleza majukumu yao kwa wageni pia wamepiga hatua kubwa katika idara ya uhamiaji bara na visiwani katika mpango wa mtandao katika utoaji wa huduma.

Tumejiridhisha kwamba mifumo yetu hapa inafanya kazi vizuri, huduma ni za haraka, na hakuna msongamano. Wageni wetu wanapata huduma kwa wakati, na usalama wao umeimarishwa kuanzia pale wanapowasili hadi kule wanapokwenda kwenye maeneo yao ya utalii na maeneo mengine nchini." Amesema Paschal.


 
Back
Top Bottom