Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Eneo la Msimbazi jijini Dar es Salaam, hususan kuanzia kituo cha mwendokasi Msimbazi hadi kituo kikuu cha mwendokasi Gerezani kupitia mataa ya Uhuru, usalama wa watembea kwa miguu upo hatarini kwa kiwango kikubwa.
Ufuatiliaji nilioufanya unabaini mambo kadhaa yanayochangia hatari hiyo kwa watembea kwa miguu.
Njia za watembea kwa miguu kuzibwa na machinga
Njia za watembea kwa miguu kwa sasa zimegeuzwa kuwa maeneo ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga. Hali hii imewalazimu watembea kwa miguu kutumia barabara zinazotumiwa na vyombo vya moto kama njia mbadala, huku barabara hizo zikiendelea kutumika kama kawaida na magari pamoja na pikipiki.
Hali hiyo imeongeza hatari kwa watembea kwa miguu, ambapo baadhi yao wamekuwa wakipata majeraha kutokana na kugongwa na vyombo vya moto wanapokuwa wanatembea. Inapotokea ajali, mara nyingi kunakuwepo na mkanganyiko, huku madereva wa vyombo vya moto wakisisitiza kuwa barabara hizo si njia rasmi za watembea kwa miguu.
Kutokana na hali hiyo, hatari imeendelea kuongezeka na baadhi ya watembea kwa miguu wameamua kuepuka kabisa kutumia eneo hilo kwa hofu ya usalama wao.
Wimbi la bodaboda na matumizi mabaya ya barabara
Katika eneo la Msimbazi Kkoo pia kuna wimbi kubwa la waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda. Wengi wao huendesha pikipiki kwa mwendo wa kasi unaohatarisha usalama wa watembea kwa miguu, hasa ikizingatiwa kuwa watembea kwa miguu hulazimika kutumia barabara kutokana na njia zao rasmi kuzibwa na machinga wanaotandaza bidhaa zao chini au juu ya meza.
Aidha, bodaboda wamegeuza baadhi ya maeneo ya barabara pamoja na njia za watembea kwa miguu kuwa sehemu za kuegesha pikipiki (parking). Hali hii inaongeza hatari kwa watembea kwa miguu wanaolazimika kutafuta njia mbadala.
Vilevile, ni hatari pia kwa bodaboda wenyewe kwa kuwa barabara hizo hutumiwa na magari, hususan mabasi ya mwendokasi. Ajali kadhaa zimekuwa zikitokea katika maeneo hayo, ambapo waathirika wakubwa wamekuwa ni watembea kwa miguu na waendesha bodaboda.
Kutozingatiwa kwa alama za zebra
Katika eneo la Msimbazi ni nadra kuona vyombo vya moto, hususan bodaboda, vikizingatia maeneo rasmi ya watembea kwa miguu kuvukia barabara. Mara nyingi hali hii imewalazimu wananchi kuvukia barabara popote pale kulingana na mazingira, jambo linaloongeza hatari ya ajali kwa watembea kwa miguu.
Zaidi ya hayo, alama za zebra ni changamoto nyingine kubwa, kwani alama nyingi zimefutika na hazionekani wazi. Hali hii inawafanya watembea kwa miguu kushindwa kutambua maeneo rasmi ya kuvukia barabara, hivyo kuongeza hatari zaidi.
Wito kwa mamlaka husika
Natambua kuwa zipo mamlaka zenye dhamana na uwezo wa kutumia rasilimali za umma kwa ufanisi ili kutatua changamoto hizi kabla athari kubwa zaidi hazijatokea. Hali ilivyo sasa inaashiria uzembe wa baadhi ya watendaji kwa kushindwa kuchukua hatua za haraka na kuweka mpangilio rafiki katika maeneo haya bila kuwaathiri wahusika.
Ni vyema mamlaka zikatafakari uwezekano wa kuweka utaratibu rafiki, ikiwemo kutenga baadhi ya njia za ndani zitakazotumika na machinga, au kufunga baadhi ya barabara zisizo muhimu ili zitumike kwa shughuli zao. Aidha, uwekwe utaratibu maalum na rafiki kwa bodaboda ili kuwaepusha na hatari za kupaki na kuegesha pikipiki katika barabara kuu.
Sambamba na hilo, alama za barabarani hususan zebra ziboreshewe na kufanyiwa upya ili ziweze kuonekana vizuri na kutumiwa ipasavyo.
Mwendelezo wa taarifa hii ~ Kariakoo: Wafanyabiashara, bodaboda wanaoziba barabara na njia za watembea kwa miguu watakiwa kupisha