Usaliti na mauaji katika mahusiano

Usaliti na mauaji katika mahusiano

Hemedy Jr Junior

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
915
Reaction score
1,082
Inauma sana ukipata taarifa kuna mtu kajiuwa kisa (Mapenzi) siwezi kujaji sana maana kuna watu wanapenda mpaka wanakuwa addicted like(Mdogo angu)

Kabla ujasalitiwa jiulize swali, mapenzi nini? swali la pili Je, upo sehemu sahihi, yaani uliyenae ndo chaguo lako au kuna mmoja alilazimisha nafsi yake?

Ukipata majibu jiulize (usaliti ni nini?). Je, nikisalitiwa nitafanya nini kwa mtu ninae mpenda?

Nadhani umeelewa kitu hapo, tuzungumzie usaliti, hutokea kwa pande zote Mwanamke /mwanaume siwezi kusema asilimia ngapi kwa jinsia gani ina saliti kwakuwa sina uhakika sana japo najua kila jinsi inaweza kusaliti

sababu zinazoweza kumfanya mtu akasaliti
1. Dharau ndani ya nyumba.
2. Huduma ndani ya nyumba.
3. Ukosefu wa amani kwa nyumba.
4. Mazoea
5. Tendo la Ndoa
6. Muda/kutompatia muda wa kutosha mpenzi wako.

Hizi ni kwa ujumla

Kwanini watu wanatoana roho kisa mapenzi? Hivi kweli mtu unayempenda unaweza kumuuwa?
Serious, watu wanaowauwa wenzi wao wanakuwa hawana amani kwenye nyumba maana hata kama ukimfumania mpenzi wako unachukuaje uamzi wa kuuwa?

Mpaka unasilitiwa kuna jambo haliko sawa kwenye Mahusiano yako/ndoa yako so jitahidi kuyaweka sawa hayo mambo yanayosababisha watu kusalitiana.

Je, utagunduaje kama unasalitiwa?
Wala usihangaike kumfutilia mtu wako kuhusu usaliti we jitahidi kutimiza kinachohitajika . Maana tatizo sio kuchat, tatizo nikumnulia vocha.

Unalalamika mpenzi wako hata kuchati hachati wakati hata vocha hujawahi mtumia. Mtumie vocha afu akikosa chati nawe upate sababu.

Mahusiano yanachangamoto kwa kwakuwa walioko kwenye mahusiano ni wanadamu so wanakosea so makosa yanatokea kwa bahati mbaya/ so kuvumiliana ila makosa yasijirudie hayo yatakuwa mazoea.

Me kwa leo elimu imeishia hapo
Uwe na siku njema.
 
Back
Top Bottom