The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Bora uchanganyikiwe wewe siku ukiulizwa na mwanao sijui utamjibu nini akuelewe ili kumjenga na kuja kuwa sehemu sahihi maishani mwake dah😓View attachment 3518866
Wanaotetea nchi yao wanaitwa majina, wachochezi, waliohongwa, wanaotumiwa na mabeberu, wahaini na kadhalika. Ajabu wanaiibiana kuiuza nchi wanajiita wazalendo,walinzi wa amani, na majina mengine mengi mazuri.
Walioko nje wakilalamika wanaitwa mawakala wa mabwana zao.
Serikali zikiishi kwa kutegemea fedha za mikopo na misaada toka kwa hao hao wanaoitwa mabwana wa wengine haziitwi nyumba ndogo ya mabwana. hawa.
Haya mambo yanachanganya.
Mwenye welewa anisaidia anifumbue mato.
Umeongea kwa uchungu sana…I feel youSimple tu. Wale walioandamana October 29 ndio wazalendo kwa sababu walifanya hivyo kupinga utawala mbovu. Haijalishi walichoma vitu au la, lengo lao lilikuwa clear. Hakuna tofauti na maandamano ya Nepal
Samia alitoa order ya kuuliwa kwa waandamanaji, huyu sio mzalendo hata kidogo. Yani yupo tayari watu wafe kuliko yeye kutoka madarakani. Huyo mama anajua kabisa watu wanamchukia na hawampendi, na anajua kabisa akijiuzulu nchi itatulia lakini hayupo tayari kujiuzulu ili tu aendelee kuwa Rais ili apate hela nyingi za bure kutoka kwenye kodi za wanaomchukia. Huyo sio mzalendo hata kidogo. Samia hajawahi kuipenda Tanzania hata kidogo, matendo yake yanaonesha
Uzalendo sio wa kila mtu, kuna watu kama Samia wamezaliwa hivyo tu basi. Hawana uzalendo wowote na hawapendi nchi zao, na kuna wengine wamezaliwa wazalendo wanatakia mema nchi yao. So ni hivyo yani, Samia ni miongoni mwa wale watu ambao hawana mapenzi na nchi zao hata kidogo, wanajijali wao na familia zao. Mambo ya taifa kwao hayawahusu