- Source #1
- View Source #1
Wakuu Salama? Katika pitapita zangu mtandao wa X nimekutana na Post hii ambayo inadai usambazaji wa umeme kwa vijiji vya Tanzania ni asilimia 100, na nimkekuwa nikisikia baadhi ya watu wakisema hilo. JamiiCheck mtusaidie hapa ni upi uhalisia?
- Tunachokijua
- Wakala wa Nishati Vijijii REA ni Taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Nishati, yenye jukumu la kuwezesha upatikanaji wa nishati bora vijijini na kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo kwa lengo la kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi vijijini. Wakala wa Nishati Vijijini, kupitia Wizara ya Nishati hufanya kazi kwakushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ofisi ya Raisi Tawala zaMikoa na Serikali za Mitaa, Wabia wa Maendeleo, Idara na Mashirika mbalimbaliya Serikali.
Kumekuwapo na taarifa inasosambaa mtandaoni kuwa usambazaji wa nishati ya umeme vijijini umefikia asilimia 100 ya vijiji vyote vya Tanzania.
Je ni upi uhalisia wa madai hayo?
Mnamo tarehe 5 Januari, 2025 na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu aliwasilisha taarifa ya hali ya upatikanaji umeme vijijini kwa Wanahabari kuelekea Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati jijini Dar es Salaam, ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2024, vijiji vilivyokuwa vimeunganishwa na umeme nchini vilikuwa 12,301 kati ya vijiji 12,318 akisema ni sawa na asilimia 99.9.
Kwa mujibu wa tovuti ya wakala wa Nishati Vijijini (REA) Januari 25, 2025 ilichapisha taarifa ikimnukuu Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu, akisema kuwa, Wakala huo umekamilisha vijiji vyote 12,318 ambayo ni sawa na asilimia 100 vimefikiwa na umeme.
Kwa mujibu wa tovuti kuu ya serikali ikifafanua muundo wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inabainisha idadi ya vijiji kuwa ni 12,318 na kwamba ilikuwa mpaka 2020.
Licha ya wakala wa nishati vijijini kubainisha kuwa umekamilisha kwa asilimia 100% ya vijiji vyote katika usambazaji wa umeme lakini bado kuna ukinzani wa idadi hiyo ya vijiji ambapo inaonesha kuna vijiji zaidi ya vinavyotajwa na wakala huo.
Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwezi Novemba mwaka 2024, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa kwa mujibu wa Notisi ya mgawanyo wa maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Tangazo la Serikali namba 769 la mwaka 2024, alitangaza jumla ya Vijiji 12,333 ambavyo vilitarajiwa kushiriki Uchaguzi huo.
Aidha kumekuwapo na maoni mbalimbali ya wananchi yanayokinzana na hoja ya kusambazwa kwa huduma ya umeme kwa asilimia 100% katika vijiji vya Tanzania wakishuhudia kuwa bado kuna baadhi ya vijiji ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo. Rejea hapa, hapa na hapa