Elections 2010 Usanii wa JK - amteua kijana aliemaliza chuo kuwa DC

Elections 2010 Usanii wa JK - amteua kijana aliemaliza chuo kuwa DC

Hao uliowataja ndugu yangu wamegombea na wananchi wenyewe wamewachagua tofauti na mtu wa kuteuliwa kiuswahiba na JK hoja yako haiingi kwenye hii tuhuma

sasa ni zamu kuwapa nafasi maswahiba wa mwanae riziwani, ili nao wake nchi
 
Mimi sioni tatizo kuteuliwa kijana mdogo, hata kama kasoma nje... La msingi hapa ni kazi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

kwali tatizo hapo hata angemteua mmoja wa wana jf, shida ni mazingira yaliyotumika
kumteua huyo kijana banaaaa aaaah!!
 
Kwani kuna tatizo gani mbona Mbunge wa Mbozi Mashariki bwana D.Shilinde naye amemaliza chuo mwaka huu, dogo yule Kigoma (Mkosamali) ndiyo kwanza anaingia final yr?

Upinzani wao hakuna neno wakichaguliwa na CCM ndio kunakuwa na taabu kaka hata kama mtu akiwa na sifa hujui akinya anye kuku tu? aaah kaka usiulize maswali mengine uchune tu hawa ndio ndugu zetu tuwavumilie na tuonyeshe ushirikiano nao.
 
:embarrassed::embarrassed::embarrassed:
 
Hao uliowataja ndugu yangu wamegombea na wananchi wenyewe wamewachagua tofauti na mtu wa kuteuliwa kiuswahiba na JK hoja yako haiingi kwenye hii tuhuma

Je kabla ya kuchaguliwa na wananchi walipitishwaje na vyama vyao? waliangalia record gani? maana huyo mkuu wa wilaya mteule umesema ni mshikaji wa JK je hao unaowasema walipataje hizo fursa na je hawana ushikaji na waliowapitisha? tusiwe watu wakuendekeza majungu tuwe wawazi na wenye kufikiri zaidi.....muda tunao tubadilike
 
SALIM AHMED SALIM.....ALITEULIWA NA NYERERE akiwa na MIAKA 24
 
SALIM AHMED SALIM.....ALITEULIWA NA NYERERE akiwa na MIAKA 24

peleleza mkuu hakuwa mshikaji wake? maana mie nimeshachoka na hizi habari za watu kukurupuka! sema Sokomoko ni mshikaji wake Mahesabu wamesoma pamoja na wameoa nyumba moja Sokomoko kamuoa mama big na Mahesabu kamuoa mdogo wake mama big yaani mama small. sio unasema tu aaah sokomoko na mahesabu ni washikaji wamebebana kupeana ajira! Tuwe analytical jamani ili wengine wenye elimu za kuungaunga tuokote mamoja mamoja...............
 
Kuana habari nimeipata toka chanzo cha uhakika Ikulu JK mbali amemteua kijana mmoja kuwa mkuu wa wilaya moja huko Nyanda za juu kusini. Huyu kijana ana miaaka kati ya 30-32 na amaemaliza chuo kikuu nje ya nchi miezi 6 iliyopita hivyo kuleta maswali ni jinsi gani atakuwa na uwezo wa kuongoza wilaya. Habari za kina kuhusu uteuzi huu wa kiswahiba kama ilivyo ada ya JK kufuata....
sioni tatizo kwa sababu mkuu wa wilaya hana kazi yoyote, kwa hiyo hata awepo au asiwepo the difference is zero
 
Hoja ya Umri kwa kweli hapo hakuna. Cha Muhimu uwajibikaji....Ila namuomba Muheshimiwa Rais awe makini
 
Humu ndani kuna watu wana wivu wa kijinga na hawatapata maendeleo kamwe iwapo wataendekeza majungu na mapipa!Mwezio kapata ulaji mpe hongera wewe unaanza eti mdogo,eti kasoma nje duh,WATU WABAYA SANA.JE UNGENIFAHAMI MIMI NI NANI NADHANI UNGEHAMA HAPA JF!
ACHA WIVU FANYA KAZI UOKOE FAMILIA YAKO

:bump::whoo::hungry::A S-alert1:😱 Kaazi kweli kweli naona tunatishana sasa.
 
hata Nyerere alimteua salim Ahmed Salim Kuwa Balozi akiwa na miaka 18 tuu! huna hoja1 kwanza mtu mwenyewe na Cv yake huijui kwanini umuhukumu kuwa hana uwezo? mtachanganyikiwa sana mwaka huu!
So what? mnataka turudi zama za ujima?
 
Makamanda wa Republican Guard (Ooops!! Green Guard) wameanza kulipwa fadhila.

Inawezekana huyo alikuwa Sajenti.
 
Kazi ya mkuu wa wilaya ni hata mtu wa darasa la saba anaweza kufanya. Kimsingi mkuu wa wilaya hana kazi ni mtu wa kufungua tu warsha. Kazi za wilaya zinafanywa na mkurugenzi, meya, madiwani na watendaji wa vitengo sio mkuu wa wilaya
 
Humu ndani kuna watu wana wivu wa kijinga na hawatapata maendeleo kamwe iwapo wataendekeza majungu na mapipa!Mwezio kapata ulaji mpe hongera wewe unaanza eti mdogo,eti kasoma nje duh,WATU WABAYA SANA.JE UNGENIFAHAMI MIMI NI NANI NADHANI UNGEHAMA HAPA JF!
ACHA WIVU FANYA KAZI UOKOE FAMILIA YAKO

Pumba!

Hivyo vyeo vya kugaiana kama njugu, ni kodi zetu hizo, so, kila mlipa kodi anayo haki ya kuhoji apatiwe maelezo nadhifu ni kwa vipi kodi yake inatumika. Dr.Mkwere na trupu lake,wangekuwa ni kampuni binafsi, we would not be having this conversation. Sijaona uhusiano wa hizi teuzi zisizo na kichwa wala miguu, na wivu au kufanya kazi kwa bidii. Kama kazi hiyo ingekuwa inatolewa based on competitive merits, hapo kusingelikuepo na sababu ya kuhoji perhaps kuhusu utendaji kazi wa mzungumziwaji.
 
Kuana habari nimeipata toka chanzo cha uhakika Ikulu JK mbali amemteua kijana mmoja kuwa mkuu wa wilaya moja huko Nyanda za juu kusini. Huyu kijana ana miaaka kati ya 30-32 na amaemaliza chuo kikuu nje ya nchi miezi 6 iliyopita hivyo kuleta maswali ni jinsi gani atakuwa na uwezo wa kuongoza wilaya. Habari za kina kuhusu uteuzi huu wa kiswahiba kama ilivyo ada ya JK kufuata....

Mimi ninachoamini siku zote mtu alienda shule na yuko commited hata kama hana experience na hiyo kazi najua ataifanya vizuri sana. siamini kabisa katika kutoa ajira ambazo si za u-CEO kuwa lazima uwe na ujuzi miaka 3-5 au zaidi.

kama huyo kijana ameenda shule vizuri hana vyeti fake kama vya kina Mary Nagu, Kamala, Lukuvi n.k ataweza kazi ya ukuu wa wilaya, sasa mazingira gani yametumika kumpa hiyo kazi si hoja sana maana kuna watu wanauzoefu miaka 20, wanaeleweka lakini wakipewa kazi hata U-DC anaboronga mpaka unapata kinyaa
 
Kwani kuna tatizo gani mbona Mbunge wa Mbozi Mashariki bwana D.Shilinde naye amemaliza chuo mwaka huu, dogo yule Kigoma (Mkosamali) ndiyo kwanza anaingia final yr?

/QUOTE]

UNAJUA MAANA YA KUTEULIWA NA KUCHAGULIWA SAMAHANI KWA HILI???THEN HUYO MBUNGE KATEULIWA AMA KACHAGULIWA TUPUNGUZE UCHAKACHUAJI
 
Kwa Mkuu wa Wilaya ana kazi gani maana zaidi ya kuwapokea Salama Kikweta, Riziwani, Makamba, Miraji, Khalfan na Januari! Nilisahau na kusindikiza MWENGE

Gottee you very right!
Hakuna haja ya kuwa na wakuu wa wilaya, mkurugenzi wa maendeleo wa wilaya anatosha. Hawa sasa kazi yao ni kutafutia vimada hawa viongozi wakitembelea wilaya na mikoa, mzigo wa kuwalipa tunabeba sisi wananchi.. kazi tunayo.:embarrassed::embarrassed:
 
Sioni tunachokijadili hapa kwa sababu hata habari yenyewe ni ya kubuni tu. Waste of time and resources. Funga thread haina maana.
 
Back
Top Bottom