Pre GE2025 Useful pointers to CHADEMA: Civil disobedience and passive resistance

Pre GE2025 Useful pointers to CHADEMA: Civil disobedience and passive resistance

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CHADEMA,

Kwa vile sasa mmeshakiri rasmi kwamba CCM wamewacheza [played you], hamna budi kujaribu mbinu nyinginezo katika harakati zenu za kuleta mabadiliko ya kisiasa.

Civil disobedience na passive resistance.

Hamasisheni watu waanze kugomea matendo ya serikali ya CCM.

Mifano:

1. Msishiriki kabisa chaguzi zozote zile zilizopangwa kufanyika chini ya mazingira yaliyopo hivi sasa. Wahamasisheni na watu waache kushiriki. Wahamasisheni waache kujiandikisha kupiga kura. Pia, vishawishini na vyama vingine vya upinzani visishiriki kabisa katika chaguzi zozote zile.

2. Washawishini wananchi waache kujitokeza kwenye sherehe zozote zile zilizoandaliwa na serikali.

3. Washawishini wananchi waache kujitokeza kwa wingi sehemu ambazo viongozi wa CCM wanakuwepo. Mfano, kama Rais ana ratiba ya kwenda kufungua mradi sehemu, wananchi wasiende. Wamwache rais na maCCM wenzake washiriki peke yao.

4. Natamani sana waajiriwa wote wa serikali kufanya migomo inayolenga kuipa shinikizo serikali ya CCM ili yapatikane mabadiliko ya kweli ya kisiasa.

Mbinu zingine mtachangia na wengine. Ila ni lazima ziwepo kwenye wigo wa civil disobedience na passive resistance.

Natambua kwamba kuyatimiza yote hayo si kazi rahisi, hususan kwenye hii jamii yetu ambayo imejaa uoga wa kupitiliza.

İli yote hayo yatimie, ni lazima wengi wetu tuwe on-code. Bila ya kuwa codified, hakuna kitakachotimia.

Kwa wale waliopo Marekani, nawatakia siku njema ya malum ziko ya sikukuu ya MLK Jr. hapo kesho Jumatatu tarehe 16.

Binafsi ninamkubali sana MLK Jr. He was super brilliant.

MLK day ndo imenipa hamasa ya kufungua mjadala huu kwa sababu Dr. King na wenzake walitumia hizo mbinu za civil disobedience na passive resistance katika kuishinikiza serikali ya Marekani kuufuta ubaguzi wa rangi wa kitaasisi [institutional racism].

Mwamko huo wa kuipa shinikizo serikali ya Marekani ulichochewa na mwanamama Rosa Parks ambaye siku moja anatoka kazini akiwa amechoka, alikataa kuachia siti yake kwenye basi ili kumpisha mzungu akae kama ambavyo sheria ilivyokuwa inasema.

Kukataa kwake huko ndo kukazaa Montgomery Bus Boycott iliyodumu kwa mwaka mzima. Mgomo huo pia ndo uliomweka Dr. King kwenye chati za uanaharakati na mengineyo yaliyobaki yakawa ni historia.

Mgomo huo pia ulipelekea mahakama ya upeo ya Marekani [US Supreme Court] kutoa uamuzi kuwa sheria za jimbo la Alabama na za mji wa Montgomery zilikuwa zinaenda kinyume na katiba ya nchi.

Pata picha endapo watu wanagoma kupanda ndege za ATCL. Wanagoma kupanda mwendokasi, n.k., mwisho wa siku serikali haitakuwa na jinsi zaidi ya kuwasikiliza watu kwa umaanani.

Najua kuandika tu na kutoa mawazo huku umekaa nyumbani kwenye kiti chako ni rahisi zaidi kuliko kutenda.

Lakini pia, hakuna tendo la kibinadamu linalotokea tu bila kuanza kama fikra kichwani.

Katika jitihada za kuleta mabadiliko nchini, ni lazima kujaribu mbinu mbalimbali.

Civil disobedience na passive resistance ni mbinu ambazo zimeleta mabadiliko sehemu nyingi tu hapa duniani.

Na kama huko kwingine mafanikio yalipatikana, basi naamini hata hapa Tanzania inawezekana pia.
Takataka wewe na mada hii
 
Acha kujipa ukipofu wa akili na macho wewe. Watanzania wana imani kubwa na serikali yao ya CCM pamoja na viongozi wake.wataendelea kumiminika na kufurika kwa wingi katika mikutano na sherehe mbalimbali.hii ni kutokana na imani kubwa waliyonayo kwa Mheshimiwa Rais na serikali yake pamoja na chama cha Mapinduzi.hii inachagizwa na kuchochewa na kazi kubwa iliyofanywa na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi.watanzania wanaona namna serikali yao inavyowekeza mabilioni ya pesa katika miradi mbalimbali ya kimkakati na kiuchumi inayotoa na kuleta fursa mbalimbali.

Watanzania wanaona namna hali ya uchumi inavyoendelea kuimarika na kumgusa kila mtanzania.watu wanajionea mzunguko wa pesa mitaani ulivyo wenye afya na kuleta matumaini. Kikubwa ni wewe kufanya kazi na kujituma kwa nguvu zako zote na siyo kusubiri kuletewa kila kitu mezani pako huku wewe ukipiga porojo mitaani.
Watanzania hawa ndio wana imani na ccm ?

FB_IMG_1575390806699.jpg
FB_IMG_1575390800494.jpg
FB_IMG_1575390792397.jpg
 
Gomea wewe na wajinga wenzio lakini nchi itakwenda na mambo yatasonga kama kawaida tu.watanzania wanajionea juhudi,uchapa kazi na ufanisi wa serikali yao katika kuwaletea maendeleo na kuweka mazingira wezeshi kwa kila mtu kuweza kutimiza ndoto zake. Hakuna maendeleo yatakayokuja kwako ikiwa hutakunjua mikono yako na kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa na kujituma kwa nguvu zako zote.kazi ya serikali ni kuweka mazingira wezeshi kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa sasa ,.jambo ambalo limepelekea Watanzania wengi kuiunga mkono serikali yao.
Kwani kuna kipindi ambacho walionyesha kutounga mkono serikali?
 
Uongozi wa Chadema mzilete kwanza familia zenu toka Ughaibuni.!

Uongozi huwa ni kuonyesha Njia.uongozi huwa ni pamoja na kusimamia yale mnayowaaminisha mnaowaongoza kwa vitendo.
Sasa Chadema kupitia mwenyekiti wake Ndugu Aikael Freeman Mbowe,mmewatangazia watanzania kuwaomba wawaunge mkono katika maandamano yenu kutaka mapendekezo yenu yaingizwe kwenye marekebisho ya katiba mpya.
Ni ukweli kwamba mnayo hoja ya msingi na mnapaswa kusikilizwa.

Ombi langu kwenu enyi viongozi waandamizi wa Chadema ni moja tu.

Kwamba muwalete na nyinyi watoto wenu wanaokula maisha huko ughaibuni pamoja na wake zenu.
Ili waje tushirikiane kwenye hayo maandamano,badala ya nyingi kutska kuwatumia watoto,wamama na wababa wa wenzenu.
Huku wa kwenu mmewaficha ulaya.
Mbowe- familia iko USA [emoji631].
Lema-familia iko Canada [emoji1063].
Lissu-familia iko Belgium [emoji1045].

Lakini pia niwaulize Chadema kwamba mlikuwa wapi kwenye kutetea ugumu wa maisha uliosababishwa na uongozi huu?
Ina maana leo ndio mnaisikia Tozo ya miamala,mfumko wa bei,kupanda nauli nchini pamoja na kutamalaki kwa ufisadi nchini?

Mlikuwa wapi kuitisha maandamano ya kupinga hayo?
Maana kiuhalisia hayo ndiyo madhila makuu ya wananchi.

Sasa nyingi mnataka wananchi wawatetee kutafuta katiba,ili na nyinyi iwape upenyo kuingia ikulu kufaidi.

Lakini mnasahau kwamba ni hivi majuzi tu mliwatenga kina Mwabukusi na Dk Slaa kwenye sakata la bandari ile DP-WORLD.
Na mkawazimia simu kabisa ilhali mlikwisha waahidi kutumia platform yenu!

Lakini pia no nyie mnaoo ngoza kwa kujitenga na vyama vinginevyo vya upinzanitt77766 nchini mkiwakejeli kwamba ni vyama vidogo.
Iweje leo mnawaomba ushirikiano??
U u 68,000 I u
 
CHADEMA,

Kwa vile sasa mmeshakiri rasmi kwamba CCM wamewacheza [played you], hamna budi kujaribu mbinu nyinginezo katika harakati zenu za kuleta mabadiliko ya kisiasa.

Civil disobedience na passive resistance.

Hamasisheni watu waanze kugomea matendo ya serikali ya CCM.

Mifano:

1. Msishiriki kabisa chaguzi zozote zile zilizopangwa kufanyika chini ya mazingira yaliyopo hivi sasa. Wahamasisheni na watu waache kushiriki. Wahamasisheni waache kujiandikisha kupiga kura. Pia, vishawishini na vyama vingine vya upinzani visishiriki kabisa katika chaguzi zozote zile.

2. Washawishini wananchi waache kujitokeza kwenye sherehe zozote zile zilizoandaliwa na serikali.

3. Washawishini wananchi waache kujitokeza kwa wingi sehemu ambazo viongozi wa CCM wanakuwepo. Mfano, kama Rais ana ratiba ya kwenda kufungua mradi sehemu, wananchi wasiende. Wamwache rais na maCCM wenzake washiriki peke yao.

4. Natamani sana waajiriwa wote wa serikali kufanya migomo inayolenga kuipa shinikizo serikali ya CCM ili yapatikane mabadiliko ya kweli ya kisiasa.

Mbinu zingine mtachangia na wengine. Ila ni lazima ziwepo kwenye wigo wa civil disobedience na passive resistance.

Natambua kwamba kuyatimiza yote hayo si kazi rahisi, hususan kwenye hii jamii yetu ambayo imejaa uoga wa kupitiliza.

İli yote hayo yatimie, ni lazima wengi wetu tuwe on-code. Bila ya kuwa codified, hakuna kitakachotimia.

Kwa wale waliopo Marekani, nawatakia siku njema ya malum ziko ya sikukuu ya MLK Jr. hapo kesho Jumatatu tarehe 16.

Binafsi ninamkubali sana MLK Jr. He was super brilliant.

MLK day ndo imenipa hamasa ya kufungua mjadala huu kwa sababu Dr. King na wenzake walitumia hizo mbinu za civil disobedience na passive resistance katika kuishinikiza serikali ya Marekani kuufuta ubaguzi wa rangi wa kitaasisi [institutional racism].

Mwamko huo wa kuipa shinikizo serikali ya Marekani ulichochewa na mwanamama Rosa Parks ambaye siku moja anatoka kazini akiwa amechoka, alikataa kuachia siti yake kwenye basi ili kumpisha mzungu akae kama ambavyo sheria ilivyokuwa inasema.

Kukataa kwake huko ndo kukazaa Montgomery Bus Boycott iliyodumu kwa mwaka mzima. Mgomo huo pia ndo uliomweka Dr. King kwenye chati za uanaharakati na mengineyo yaliyobaki yakawa ni historia.

Mgomo huo pia ulipelekea mahakama ya upeo ya Marekani [US Supreme Court] kutoa uamuzi kuwa sheria za jimbo la Alabama na za mji wa Montgomery zilikuwa zinaenda kinyume na katiba ya nchi.

Pata picha endapo watu wanagoma kupanda ndege za ATCL. Wanagoma kupanda mwendokasi, n.k., mwisho wa siku serikali haitakuwa na jinsi zaidi ya kuwasikiliza watu kwa umaanani.

Najua kuandika tu na kutoa mawazo huku umekaa nyumbani kwenye kiti chako ni rahisi zaidi kuliko kutenda.

Lakini pia, hakuna tendo la kibinadamu linalotokea tu bila kuanza kama fikra kichwani.

Katika jitihada za kuleta mabadiliko nchini, ni lazima kujaribu mbinu mbalimbali.

Civil disobedience na passive resistance ni mbinu ambazo zimeleta mabadiliko sehemu nyingi tu hapa duniani.

Na kama huko kwingine mafanikio yalipatikana, basi naamini hata hapa Tanzania inawezekana pia.
Ngabu una akili sana.

Kususia ni silaha ya kimyakimya
 
Ccm imeshakuwa mhimili wa 4 wa nchi, tena wenye mamlaka kuliko mihimili yote.

Katiba mpya pekee ndiye itakayoweza kusawazisha hilo.
CCM huwa hawajuai kwamba kuna KATIBA nchi hii, ukiwasikiliza vizuri huwa hawataji katiba mahala popote. Utawasikia TUMETEKELEZA ILANI ya CHAMA ya 2020 sijui 2021 na kadhalika . CCM wao ILANI ya CCM ndiyo katiba. Lisemwalo kwenye hiyo ilani hata kama ni KUUA lazima litekelezwe.
 
Watanzania siyo wajinga kama unavyofikiria wewe kwa mawazo ya kijinga na yasiyo na mantiki wala mashiko. Ni nani na mtanzania yupi mwenye akili timamu na anayejitambua na anayefahamu na kutambua historia ya CHADEMA,matendo ya viongozi wa CHADEMA na kukosa kwao uzalendo kwa Taifa letu? Watanzania kwa mamilioni yao wanafahamu kuwa viongozi wa CHADEMA siku zote wamekuwa wakipigania maslahi yao.siki zote wamekuwa waumini wa kutafuta upenyo wa sheria au kanuni au mazingira yatakayowawezesha kupata nafasi za uongozi hasa ubunge ili wakapata pesa za kushibisha matumbo yao. Ni wapi katika muda wote umewahi kusikia viongozi wa CHADEMA wakikataa posho wakiwa bungeni au kusema wanaitisha maandamano ya kupinga posho za wabunge kipindi chote walipokuwa bungeni?

Kwanini hatujawahi kuona CHADEMA wakipinga kiinua mgongo kwa wabunge kisicho na kikokotoo kama ilivyo kwa watumishi wengine kama walimu na maaskari? CHADEMA hawajawahi kufanya haya kwa kuwa yalikuwa yanawanufaisha na kuwapa shibe ya matumbo yao na kutunisha akaunti zao kama ambavyo akina sugu wamekuwa wakijitapa kuwa na fedha nyingi kwenye akaunti zao benki.

Watanzania hawawezi kushiriki wala kuunga mkono huo ujinga uliouopendekeza kwa sababu CHADEMA hawana usafi wa kuwashawishi watanzania kufanya hayo. Watanzania wanaaelewa dhamira njema ya Rais wao na serikali yao katika kuwainua kiuchumi.wameona na kujionea namna ambavyo miradi mbalimbali imetekelezwa hapa nchini na kuwasogezea huduma karibu yao Watanzania wameona namna mabilioni ya fedha yalivyoelekezwa katika miradi mbalimbali iliyogusa maisha yao na kuleta matokeo bora na chanya.watanzania wanajionea namna Rais wao na serikali yao inavyopambana usiku na mchana kuboresha maisha yao kwa kuelekeza kila senti inayokusanywa katika shughuli zinazozalisha fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwepo ajira kwa vijana,kuongezeka kwa mapato, kuchochea biashara na uwekezaji, kuongezeka kwa mzunguko wa pesa mitaani na mengine mengi tu.
Je unadhani hao CCM unao watetea nao ni wasafi 🐩?
 
Ujinga ni mtaji wa wanasiasa Tanzania. Mtaji kwa watawala na hao wengine.

Tusingekuwa wajinga lowasa asingepewa kugombea urais chadema 2015, hakuwa na sifa za kuiwakilisha chadema.
Lowasa ni Mtanzania kama Watanzania wengine yeye alikuwa kiongozi mmoja wapo tu ktk serkali ya CCM na maamuzi hakuwa anatoa yeye peke yake kwahiyo kumtuhumu yeye kama yeye ni makosa tuhumu system nzima ya wakati huo.
 
Back
Top Bottom