Mwl Philemon
Member
- Nov 29, 2018
- 63
- 70
Kwa yanayoendelea sasa kwenye mpira wetu ni ujinga na upumbavu mkubwa kuoneshwa na wapenda maendeleo ya michezo hususan huu mchezo pendwa wa mpira wa miguu.
Ndani ya siku tatu kumekuwa na matukio yasiyo ya kuvutia kwa wanamichezo wa kweli. Lilianza la Ali kamwe kumshambulia kwa maneno ya kejeli Kocha Juma Mgunda jambo ambalo si la kimchezo. Kama Ali ana chuki binafsi na Mzee yule angetafuta namna nyingine kumtusi au kufikisha ujumbe wake si Timu yetu pendwa.
Na pili ni hili la Mashabiki wa soka kushangilia kwa furaha kifo cha shabiki mwingine kisa ni shabiki wa timu nyingine huu si mchezo wala utani wa jadi bali ni uadui na chuki inayoendelea kujengeka ndani yetu. Lisipokemewa litakuja kuleta maafa makubwa baadaye.
Tubadilike huu ni ushamba katika michezo. Kama huna cha kufurahia kwenye mechi fulani achana nayo. Kama huna cha kujifunza kwa mwingine achana nae.
Haya majibizano ni upuuzi mtupu.