Ushabiki wa Yanga na Simba unatawaliwa na ujinga, uswahili, kujipendekeza plus uzuzu

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Niliwahi sema hapa ukitaja wapinzani wa Jadi Duniani Simba na Yanga haziwezi fikia hata robo ya upinzani wa timu za Agentina au hata hopo Misiri.

Shida ni kwamba wale ni wasomi, hio ndo tofauti, Tanzania kwanza asilimia 80 ya mashabiki wa hizi timu ni waswahili, ambao elimu ni shida baada ya hapo sasa njoo kwenye mfumo wa nchi wa kujipendekeza.

Yaani kwa sasa Yanga na Simba zi ashindana kuwafuarahisha wakuu wa nchi yaani kwba nani anawafurahisha zaidi, hiki ndio wanacho kifanya.

Kwa kifupi mimi nilikuwa shabiki wa yanga ila nimeacha sitaku kuwa sehemu ya wajinga kwenye nchi hii.
 
Hili jambo mm linanikera sana eti kwenye matamasha au mechi wanakuja viongozi wa kichama wakati wengine mambo ya siasa yanatuboa kweli,

Upinzani wetu hamna kitu hatujafika levo za kina Zamaleki mfano ile mechi ya Simba na Zamalek mwaka 2003 Alhyl pamoja na upinzani wao wote hawawezi kumpa mbinu mpinzani anaecheza na Zamaleki ila ile mechi baada ya zamaleki kutolewa basi Al Ahyl waliwacheka sana na kuwatania zamaleki kuwa wamfungwa na timu inawachezaji wadogo under 21 ila huku vice versa.

Ukienda kwa mashabiki hao ndio hamna kitu kabisa yaan Yanga akifanya vizuri mashabiki wa Simba watapinga hata kama kuna ukweli na Pia Simba akifanya vizuri Yanga watapinga hata kama kuna ukweli na hawa mashabiki ndio mazuzu kwa asilimia kubwa wengi wanapenda udaku umbeya kuona kila siku timu zao zinasifiwa ukiziponda hata kama zimekosea watakuchukia.

Mwisho wachambuzi ndio hamna wanapewa hela ili kusifia tuu
 
Niliwahi sema hapa ukitaja wapinzani wa Jadi Duniani Simba na Yanga haziwezi fikia hata robo ya upinzani wa timu za Agentina au hata hopo Misiri...
Endelea tu kuishi maisha yako mkurugenzi. Haya ya ushabiki wa Yanga na simba, tuachie sisi waswahili ambao hatuna elimu.
 
Adui mkubwa wa hili taifa ni ujinga na mbaya zaidi hizi shule zetu za kata zimeshindwa kutoa ujinga.Hata ukiangalia namna hawa mashabiki wanavyochangia mada humu JF au wanaoanzisha nyuzi humu utajua namna taifa lilivyojaa wajinga
Niliwahi sema hapa ukitaja wapinzani wa Jadi Duniani Simba na Yanga haziwezi fikia hata robo ya upinzani wa timu za Agentina au hata hopo Misiri...
 
atuache na huu ulevi wetu wa Simba na Yanga.
Endelea tu kuishi maisha yako mkurugenzi. Haya ya ushabiki wa Yanga na simba, tuachie sisi waswahili ambao hatuna elimu.
mtani nasikia mnampango wa kupora mchezaji Singida Big stars?
 
atuache na huu ulevi wetu wa Simba na Yanga.mtani nasikia mnampango wa kupora mchezaji Singida Big stars?
Ikitokea hivyo litakuwa ni jambo jema. Maana hata nyinyi pia mlimpora Habib Kiyombo kutoka hapo hapo Singida Big Stars baada ya kupanda dau.
 
Yaani hata ukiamua usiwe mshabiki wa timu hizi,haikuweki mahali salama kuwa wewe si mmoja wapo katika wajinga wengi wa Tanzania,Bali wewe utakuwa mjinga aliyejitenga na mpira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…