Ushahidi: Maisha tena baada ya kifo


Mkuu siwezi kukuamini moja kwa moja japokuwa mimi huwa kinanikutaga kitu kimoja ambacho huwa kinanishangazaga sana....

Ni kwamba kuna locations na mahali flaniflani ambapo huwa nilisha zionaga au kujihisi niliwahi kuwa mahali hapo lakini ukweli ni kwamba huwa sikuwahi kufika maeneo hayo.

Sasa inapotokea nafika na kufanya kitendo flani ambacho nilishawahi kukifanya huwa nakumbuka nilisha wahi kufika mahali hapo na kufanya kitendo hicho japokuwa inakuwa sio kweli.

Maswali ambayo najiulizaga huwa naziotaga hizo sehemu ndipo nafika? lakini ukweli ni kwamba si ndoto yanakuwa kama maono flani ivi...Huwa naishia kuhamaki tu!
 
sijaona USHAHIDI wa maisha baada ya kifo
Hiki ni kipengele tu
Kama chambi chambi waweza tafuta
info kuhusiana na majambo haya ukapata kupanua
namna yako pamoja nanihii,kufikiri.
 
You're very right mkuu.
Ukisema hivyo mie nakuelewa sawiha,
Ni kwamba hili somo ni pana sana,
hicho unachokiona ni kipengele cha
''Deja vu''.Ambacho ni kiashiria tosha kwamba
Wewe ulikuwepo kabla na utakuwepo baada.
 
Ujinga katika ubora wake.
Wewe hapa duniani ni mgeni.
Kwenye Avatar naona kuna neno Jesus.
je? unamfahamu?
Basi na yeye huwa anakufa na anarudi tena.
''After a certain period of time.''
Hata aliyembatiza ni Eliya ambaye alipaa na akaja kuzaliwa kama Yohana.
Hata huyo Jesus alikuwepo kabla ya kuuvaa mwili(yaani kabla ya kuzaliwa na bikira mariam).
Enzi za Musa aliingia kwenye ile Fimbo ya shaba ambaye kila aliye ng'atwa na nyoka mwenye sumu ya kufisha.
Alipoiangalia ile Nyoka kwa imani hakufa.
Ukishakufa utakumbuka haya.
 
Mkuu hata mimi hili linanitokea najikuta nipo sehemu na vitendo vinavyofanyika sawa na vitu ambavyo ninauhakika kuwa navijua au nilishafika lakini najikuta kwa fikra ya kawaida sajawai kufika hapo! Sijui nini aisee!
 
Kama mnajua kuwa mtu akifa anakuja kuzaliwa upya mbona msijue siku zenu za kufa?kuna mambo mengine mtu hutakiwi kudadisi wala kijua maana hayana msaada yoyote katka maisha tunayoishi dunian
 
You're very right mkuu.
Ukisema hivyo mie nakuelewa sawiha,
Ni kwamba hili somo ni pana sana,
hicho unachokiona ni kipengele cha
''Deja vu''.Ambacho ni kiashiria tosha kwamba
Wewe ulikuwepo kabla na utakuwepo baada.

It's Deja vu all over again
 
Mkuu kabla ya kuangalia hayo matukio ambayo unayaita ni ushahidi ningependa kujua msingi wa hiyo Imani ni upi? Mfano watu wenye kuamini kuwa mtu akifa harudi tena ulimwenguni hadi hiyo siku ya mwisho ambayo watafufuliwa viumbe wote,watu wenye imani msingi wao ni kwa Mungu,kwa maana kwamba wao wanaamini mungu na mungu ndiye aliyesema hivyo.

Tuanze hapo kwanza.
 
Kama mnajua kuwa mtu akifa anakuja kuzaliwa upya mbona msijue siku zenu za kufa?kuna mambo mengine mtu hutakiwi kudadisi wala kijua maana hayana msaada yoyote katka maisha tunayoishi dunian
Haya mambo yana msaada sana katika maisha.
Hasa katika kipengele cha "karma" vilevile laana na baraka.
 
nilikuja kwa shauku..... utumbo mtupu
 
Nashukuru kwa swali lako zuri.
Msingi wa hili jambo hauegemei kwenye imani yeyote,
bali ni utafiti uliofanywa na taasisi kadhaa ulimwenguni.
ikiwemo Stony Brook University.
 
Nashukuru kwa swali lako zuri.
Msingi wa hili jambo hauegemei kwenye imani yeyote,
bali ni utafiti uliofanywa na taasisi kadhaa ulimwenguni.
ikiwemo Stony Brook University.

Mkuu huo utafiti ulifanywa baada ya kuwepo hiyo Imani au vp? Maana navyojuwa kuwa hiyo Imani imesambaa sana huko Asia hasa wahindi ndiyo imani yao hiyo kubwa.
 

mkuu mbona dizaini kama ulishakufa vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…