Ushahidi wa Jinsi Mihimili ya Kenya ilivyo huru kulinganisha na ile ya Tanzania huu hapa

Ushahidi wa Jinsi Mihimili ya Kenya ilivyo huru kulinganisha na ile ya Tanzania huu hapa

nadhani hukufuatilia siasa za Gachagua na nadhani huelewi mashtaka ma5 yaliyomtia hatiani kwenye bunge la seneti...

kuugua kwake ni mikakati na mbinu ya eti mahakama itamnusuru...
Atasagwa vizuri sana hiyo Oct 24[emoji205]
Huna unacho jua kabisa we endelea kusikiliza TBC taifa, mimi niko Nairobi jnacho ongelea nakiona live wewe uko mbagala unataka kunielewesha mimi.
 
Pamoja na kwamba Bunge la Kenya limemuondoa Madarakani Naibu wa Rais aitwaye Gachagua, Na kufikia hata kumpitisha Naibu Mpya aliyeteuliwa na Rais William Ruto, Lakini shughuli yote hiyo imezimwa na Mahakama ya Nchi hiyo.

Hii ni Baada ya Bwana Gachagua kuwasilisha pingamizi Mahakamani, Akipinga kuondolewa kwake kwa alichodai hakukufuata Utaratibu, Mchakato huo utaendelea baada ya Mahakama kusikiliza kesi hii iliyofunguliwa kwa hati ya dharula, na kama Mahakama hiyo itakubaliana na madai ya Gachagua aweza kurejeshwa Madarakani.

Jambo hili haliwezi kufanyika Nchini Tanzania, Haingewezekana kwa namna yoyote ile hata ikibidi kwa gharama ya Majaji na Gachagua mwenyewe kupotea ama kutekwa, Kwa Tanzania kauli ya Viongozi ina nguvu kuliko Amri Kuu za Mungu (Mifano ya Jambo hili tukiiweka hapa basi JF itajaa)

Soma Pia:
Kwa kadri ya Maono yangu Kenya haikupaswa kuwemo kwenye Jumuiya ya Africa Mashariki, kulikojaa viongozi Madikteta wasioheshimu Katiba walizoapa kuzilinda tena kwa kushika vitabu vya dini zao kwenye mkono wa Kulia.

Nitajaribu kuishawishi Kenya ijiondoe kwenye Jumuiya ya Africa Mashariki ili kulinda Heshima yake

Mungu Ibariki Jamhuri ya Watu wa Kenya
Imewasaidia nini wakenya .? Kila siku wanauana sababu ya hiyo so called democracia walijiwekea .

Wanapiga hatua kumi mbele mwaka mmoja wanarudi 20 nyuma ndani ya siku moja .
 
Nikikumbuka mlichomfanya Ndugai sina hamu
haiwezekani kama nchi au serikali yenye uelekeo, malengo na dhamira moja, halafu anajitokeza mwenye kiburi moja kati yenu akiwa na nia au mipango ya kuhujumu, kutatiza au kubeza malengo yale...

kisiasa ni Lazima atolewe kwenye nafasi yake, ili apate fursa akafanye hayo akiwa nje ya mfumo ili malengo yafikiwe na wengine...

kumbuka,
there is two constants in politics,
Interest and Betreyal 🐒
 
Back
Top Bottom