Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mashahidi upande wa Jamhuri katika Kesi Namba Cc 32444/24 inayomkabili Saleh Ayoub (39) Mkazi wa Salasala Jijini Dar es Salaam, Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres iliyopo Mbezi - Africana anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi wake wanatarajiwa kuanza kutoa ushahidi Februari 6, 2025.
Kesi hiyo ambayo imeendelea kwa kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Januari 16, 2025, Wakili wa Jamhuri, Harrison Lukosi ameiomba Mahakama kuridhia kufanya marekebisho kwenye Hati ya Mashtaka kuhusu marekebisho ya tarehe ambazo mtuhumiwa anadaiwa kutenda tukio, ambapo Mahakama imekubali ombi hilo na kuiahirisha kesi hiyo hadi Februari 6, 2025 kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi.
Ikumbukwe Jamhuri ilieleza mbele ya Mh. Hakimu Mkazi Mkuu, Hawa Magesa ambaye anasikiliza kesi hiyo kwamba watakuwa na Mashahidi sita ambao wanatarajiwa kutoa ushahidi kwa upande wao.
Upande wa utetezi katika kesi hiyo unaongozwa Wakili Faraji Mangula.
Itakumbukwa mshtakiwa alipandishwa kizimbani siku moja baada ya Mwanachama wa Jamiiforum.com kueleza madai yaliyomuhusisha mtuhumiwa huyo na kuhoji sababu za kutochukuliwa hatua stahiki za kisheria.
Kusoma hoja ya awali ya Mwanachama huyo bofya hapa ~ Walimu wa Shule ya Green Acres (Dar) wanaotuhumiwa kulawiti na kuwadhalilisha Wanafunzi, wanalindwa na nani?
Pia soma:
~ Watu 6 kutoa ushahidi Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake
~ Dar: Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi wake afikishwa Mahakamani
~ Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres anayetuhumiwa kulawiti Mwanafunzi yaahirishwa Mwezi mzima, Hakimu apata hudhuru
~ Dar: Kesi ya Mwalimu Saleh Ayoub anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi yaahirishwa hadi Februari 17, 2025
~ Shahidi: Mwalimu Mkuu anayedaiwa kumlawiti Mwanangu alimwambia 'ukisema nitakupiga nikuvunjevunje'