Kwani Tanganyika ipo kwenye ramani?
Kwani Tanganyika ipo kwenye ramani?
Mada kama hizi nadhani inafaa tufike mahali tukubali yafuatayo:..Mkutano wa hadhara wa Act Wazalendo huo hapo chini.
..Tena wanatishia kuvunja muungano na kurudisha kiti cha Zanzibar Umoja wa Mataifa.
..Wakati huohuo huku Tanganyika vyama mbadala vinazuiwa kufanya mikutano ya hadhara.
..Je, zuio hili la upande mmoja wa muungano kutokufanya mikutano, huku upande wa pili wakiruhusiwa ni halali?
..Je, huu sio UBAGUZI?
Aiseeee !!..Mkutano wa hadhara wa Act Wazalendo huo hapo chini.
..Tena wanatishia kuvunja muungano na kurudisha kiti cha Zanzibar Umoja wa Mataifa.
..Wakati huohuo huku Tanganyika vyama mbadala vinazuiwa kufanya mikutano ya hadhara.
..Je, zuio hili la upande mmoja wa muungano kutokufanya mikutano, huku upande wa pili wakiruhusiwa ni halali?
..Je, huu sio UBAGUZI?
Mkuu 'Arovera', hili wazo limeniijia kichwani baada ya kuiona hiyo bendera.View attachment 2349206
Bendera ya Tanganyika hiyo hapo bado ipo mioyoni mwa watanganyika
Mimi ni mmoja wa hao "wanaopaswa kukemea...", lakini pamoja na kukemea huko ni lazima vyama vya siasa vyenyewe viwe tayari kupigania haki zao.Kalamu,
..Juzi jeshi la Polisi Mwanza liliwakamata viongozi na wanachama wa Chadema waliokuwa wakifanya maandalizi ya mkutano wa hadhara.
..Na Chadema walifuata taratibu za kupeleka taarifa Polisi lakini majibu waliyoyapata ni hayo ya kutiwa nguvuni.
..Kwa upande mwingine hatuwezi kusema kwamba Zanzibar ni tofauti na Tanganyika tunapozungumzia masuala ya vyama vya siasa na haki zao.
..Masuala ya vyama vya siasa ni ya MUUNGANO. Msajili wa vyama vya siasa ni mmoja kwa Tanganyika na Zanzibar.
..Zaidi, jeshi la Polisi linalokamata Watanganyika kwa kuandaa mikutano ya hadhara ndilo hilohilo linaloruhusu Wazanzibari kutumia haki hiyo ya kikatiba.
..UBAGUZI huu unapaswa kukemewa na kila mpenda demokrasia wa Tanzania.
Mimi ni mmoja wa hao "wanaopaswa kukemea...", lakini pamoja na kukemea huko ni lazima vyama vya siasa vyenyewe viwe tayari kupigania haki zao.
Huku Tanganyika Kinana amezunguka nchi nzima kwa kwa mgongo wa kukagua uhai wa CCM. Mimi sioni tofauti yoyote na hao ACT huko Zanzibar na hawa CCM huku Tanganyika.
Kwa hiyo ninarudi kulekule kwa vyama kama CHADEMA. Hayo waliyofanyiwa Mwanza ndiyo yangepaswa kuwa kichocheo cha kukataa kabisa kunyanyaswa huko.
Haya mazungumzo ya "maridhiano" naona yameleta madhara makubwa sana kwa hiki chama. Mbona huko siku za nyuma wakati wakisurubiwa na Jiwe, lakini waliweza kusikika kila kona ya nchi?
Ni kipi kilichotokea sasa kinachowafanya kama wamedungwa sindano ya ghanzi? Kurudishiwa mali kwa viongozi wao; jambo ambalo ni haki yao?
Inabidi sasa watu wahoji mabadiliko haya ndani ya CHADEMA yametokana na nini. CHADEMA imepoa mno, wakati ambao wanatakiwa kuwa moto hasa...Juzi jeshi la Polisi Mwanza liliwakamata viongozi na wanachama wa Chadema waliokuwa wakifanya maandalizi ya mkutano wa hadhara.
..Na Chadema walifuata taratibu za kupeleka taarifa Polisi lakini majibu waliyoyapata ni hayo ya kutiwa nguvuni.
Inabidi sasa watu wahoji mabadiliko haya ndani ya CHADEMA yametokana na nini. CHADEMA imepoa mno, wakati ambao wanatakiwa kuwa moto hasa.
Kumbuka, Samia amefanya juhudi zote aonekane yeye ni tofauti na Magufuli.
Amejitahidi aonekane ni mtu anyependa haki, mtu asiyependa kuonea watu wengine.
Sasa huku kuzuiwa kwa CHADEMA huko Mwanza inaonekana wazi kabisa kuwa ni kinyume cha anayoyataka yeye Samia.
Kwa nini CHADEMA wasitumie nafasi hiyo kuhoji dhamira ya kiongozi huyu?
Naomba sana sasa wasiishie hapo...Ninavyoelewa mimi Cdm wamekuwa wakihoji kwa muda mrefu zuio la mikutano ya hadhara.
..Pia njia mojawapo ya kuwaonyesha wananchi na dunia unafiki wa Ssh ni hiyo waliyotumia Cdm ya kutoa taarifa za mkutano Mwanza na polisi kuwazuia.
Naomba sana sasa wasiishie hapo.
Ni wakati mwafaka sasa wa kusonga mbele zaidi, na kwa kasi zaidi.
Wananchi wapo wa kutosha kabisa, kama madai ya CHADEMA ya kuwa na wanachama zaidi ya milioni (?)ngapi; na wapenzi wengi zaidi wa chama hicho...Na sisi wananchi tusonge mbele zaidi, na kwa kasi zaidi.
..Tukionyesha kwamba suala hili linatugusa tutawatia moyo Cdm kulipigania.