Ushahidi wa uchakachuaji wa matokeo wa necta waanza kuanikiwa

Ushahidi wa uchakachuaji wa matokeo wa necta waanza kuanikiwa

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,570
Necta kwa mara ya Kwanza inajikuta ikiingia katika kashfa ya kuchakachua matokeo ya Zanzibar.
Wasomi mbali mbali wa Zanzibar wameanza kuandaa Ushahidi unaonyesha Jinsi ya NECTA ilivyofanya uchakachuaji wa hali ya juu.
wanadai haijawahi kutokea popote dunia matokeo ya Mtihani wa taifa kuwa kama yalivyotolewa na NECTA.
wanadai hawezekani wanafunzi 170 kati ya 171 wafutiwe kwa pamoja mmoja tu abaki.
pia wamefika mbali na kusema kama Ndalichako anadai wazanzibar mtihani kwanini hakugundua wanafunzi wa Dar kwamba wameiba? wanadai hawezekani uibiwe zanzibar usipatike Dar , hata Mwanza.

wamesema wanandaa vitabu mbali mbali , makala kupita magazeti. tayari gazeti la Zanzibar leo limeanza kuchapisha makala mbali mbali kuonyseha Uchakachuaji wa NECTA
 
matokeo yamechakachukuliwa bara na visiwani,serikali haina gela hatuwezi waruhusu wafaulu wote tuonekane tumeshindwa kuwasomesha
 
Mkuu tupatie taarifa kamili maana sijaona kilichoanza kuanikwa ni kipi! Kama ni uchakachuaji, upi umeanza kuanikwa?
wengine tumefungua thread kwa kasi kumbe ni yaleyale malalamiko tuliyokwishayazoea...kukata kilomolomo chao, ndalichako anatakiwa awaonyeshe ***** uliofanywa na watoto wao.
 
mkuu umefaulu kwa daraja lipi, maana jinsi ulivyoandika inaonekana nawe ni mmoja wa waathirika lakini inaonekana wewe matokeo yako unayo.
 
jamani hii sasa ni too much...hata neno u.p.upu haliruhusiwi jf? kama tuko china vile.
 
Thread inamapungufu ungetoa tarifa iliyokamilika si wote wanjua kilochotokea
 
Mkuu tupatie taarifa kamili maana sijaona kilichoanza kuanikwa ni kipi! Kama ni uchakachuaji, upi umeanza kuanikwa?
Hizi ni story tunazopiga tukiwa kwenye gahawa. hazina facts wala evidence ya kuzifanya ziwe na mshiko....kama mtu anachakachua matokea ya elimu na ushahidi upo, si asulubishwe tu. Mbona ushahidi wa mambo mbali mbali unatolewa hapa kwanini huo nao usitolewe?
 
Necta kwa mara ya Kwanza inajikuta ikiingia katika kashfa ya kuchakachua matokeo ya Zanzibar.
Wasomi mbali mbali wa Zanzibar wameanza kuandaa Ushahidi unaonyesha Jinsi ya NECTA ilivyofanya uchakachuaji wa hali ya juu.
wanadai haijawahi kutokea popote dunia matokeo ya Mtihani wa taifa kuwa kama yalivyotolewa na NECTA.
wanadai hawezekani wanafunzi 170 kati ya 171 wafutiwe kwa pamoja mmoja tu abaki.
pia wamefika mbali na kusema kama Ndalichako anadai wazanzibar mtihani kwanini hakugundua wanafunzi wa Dar kwamba wameiba? wanadai hawezekani uibiwe zanzibar usipatike Dar , hata Mwanza.

wamesema wanandaa vitabu mbali mbali , makala kupita magazeti. tayari gazeti la Zanzibar leo limeanza kuchapisha makala mbali mbali kuonyseha Uchakachuaji wa NECTA

huyo mmoja atakua aliandika majibu yake kwa kadri ya uwezo wake wakati wenzake 170 majibu yao yanafanana mpaka nukta! kama kuna watu wanajiita wasomi wanahoji jambo kama hilo basi usomi wao ni janga ktk taifa jipya la Zanzibar!!
 
Huyu muanzisha mada ni mmoja kati ya vilaza maarufu wa JF ktk fani ya manung'uniko. Ndio maana kwa kujua kuwa anataraji kuongea pumba, kafungua account mpya keo na kuandika malalamiko yake.

Tumsamehe ni muhanga wa matokeo mabovu
 
Huyo mtu anaesema kuwa kama ikivuja znz ni lazima ivuje dar na mwanza atakuwa msomi kweli? Mbona haeleweki? Mi nadhani tuache majungu na fikra hasi (negative thinking) bila sababu za msingi. Tuamini kwamba wamefeli hadi atakapotokea mtu kutuletea ushahidi mbadala. Wapo form four huku mtaani hawajui kuandika hata barua. Wangefaulu vipi hawa jamani
 
Too gud a label fore a content.......................weka yaliyoanikwa ndugu
 
Back
Top Bottom