Mkuu mimi ni Simba dam dam ila tukiongea kihalisia hilp goli ni offside. Tuweke ushabiki pembeni. Labda kama wengine hatujui kutafsiri sheria ya offside.
Sasa basi, hii sheria inaangalia position ya mcheza alipokuwa wakati pass inatoka kwa aliempa assist. Ukiangalia hapo wakati Shiboub anaupiga mpira kichwa tayari beki yule alishatengeneza offside trap na Kagere akawa ameshaotea.
Mimi sio mnafki kwenye ukweli nakuwa mkweli. Simba tumeshinda nimefurahi tumeongeza point tatu. Lakini kama referee/lineman angekuwa makini au pangekuwepo VAR lile lisingekuwa goli.
Pia mashabiki wa team pinzani nawaomba mjifunze mpira. Msiilaumu Simba kwa goli lile, sana sana mlaumu waamuzi kwa kutoona hiyo offside lakini pia kabla hamjamlaumu mwamuzi mjue kuwa na yeye ni binadamu.
Kama uliwahi kucheza mpira angalau level ya kufundishwa na waalimu, tulikuwa tunasisitizwa kucheza kwa kufuata kipyenga/filimbi na sio kelele za wapinzani au mashabiki. Meddie alicheza kwa kufata kipyenga/filimbi.
Simba Nguvu Moja.