Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
Haya ni maonyesho yaliyoandaliwa na Wazungu (Umoja Wa Mataifa) kuhusu kile kilichotokea huko Ulaya wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia! Maonyesho hayo yalihusu hasa mauaji ya Wayahudi huko Ulaya!
Kilichonigusa hasa na kunifanya mpaka niandike hapa ni jinsi Wazungu walivyofanya haya maandalizi, kwanza aina ya wanafunzi waliokuja ni wa kutoka Shule za kawaida kabisa za Serikali za kata yaani Mtz wa kikawaida, lkn kama hii shughuli ingeandaliwa na Serikali yetu (sisi Watz weusi) basi Wanafunzi ambao wangepata fursa hii wangetoka Shule za binafsi kama Al Muntazir, International school, St Marys n.k yaani shule za Watoto wa kidosi!
Pili kilichonivutia zaidi kuhusu haya maandalizi yaliyofanywa ni Wazungu ni Lugha iliyotumika, Wazungu wameamua kutumia Lugha ya Kiswahili lkn kama hii ingefanywa na Mtz Mdiaspora kama John Mashaka basi lazima wangeandika kwa Kiingereza ingawaje mlengwa ni Mtz wa kawaida!
Hii imenifundisha moja ya kwamba Wazungu ni kweli kabisa wana akili sana kuliko sisi!