DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu imeendelea tena leo, Jumatatu Oktoba 06.2025 kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam chini ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru
Kesi hiyo imetajwa Mahakamani hapo leo kwaajili ya mashahidi wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao Mahakamani, na shahidi wa kwanza (1) aliyewasilisha ushahidi wake leo ni ACP George Willbert, Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, aliyetoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga
ACP George Willbert (48) alianza kwa kuieleza Mahakama kuwa mnamo Aprili 04.2025 Ofisini kwake alifika ASP Kaaya anayefanya kazi kwenye dawati la doria mtandaoni, alipofika alimueleza kuwa aliona picha jongefu kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube ya Jambo TV ambapo picha jongefu (Video) hiyo ilibeba kichwa cha habaria kisemacho "Tundu Lissu uso kwa uso na watia nia, No Reforms, No Election"
Anasema ASP Kaaya alimueleza kuwa maudhui yaliyopo kwenye picha hiyo jongefu yalikuwa na ujinai ndani yake, ndipo ASP Kaaya alipochukua simu janja yake na kuanza kumuonesha maudhui hayo ambapo akiwa anaangalia alimuona Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu akiwa anaongea
Anasema alioneshwa vipande tofauti vya hotuba ya Lissu, ambapo miongoni wa vipande hivyo alimnukuu akisema "Polisi hubeba vibegi mgongoni vyenye kura feki na kwendanavyi kwenye vituo vya kupigia kura"
Wakati ACP George akiendelea kueleza, mshtakiwa Tundu Lissu ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo alisimama na kuieleza Mahakama kuwa ushahidi unaohusu Polisi kubeba kura feki kwenye vibegi unaotolewa Mahakama hapo hauhusiani na makosa anayoshtakiwa nayo, Lissu alisema yeye ameshtakiwa kwa kusema "atakinukisha vibaya sana nk", hivyo kuomba ushahidi huo ufutwe
Wakili wa Serikali Mkuu Nassor Katuga alipinga vikali hoja ya mshtakiwa, kwa kueleza kuwa ni jukumu la Jamhuri kuthibitisha kuhusu mashtaka anayoshtakiwa mtuhumiwa, ambapo baadaye Mahakama ilikubaliana na hoja za Jamhuri na kumruhusu shahidi aendelee kutoa ushahidi wake...
Chanzo: Jambo Tv