Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
SISI WETU NI MAGUFULI, WENGINE MSITUTISHE!
Tanzania yapendeza
Amani yetu yaangaza
Uhuru wetu twajivunia
Na tisa hamsini metimia
Beberu we situtishe
Utaipata kasheshe.
Wapo wenye inda
Nia yao kulivurunda
Taifa letu imara
Watuletee madhara
Tunasema hatukubali
Tutawafyekelea mbali.
Twatimiza demokrasia
Viongozi kujipatia
Kwa njia za haki na amani
Kupata walokuwa makini
Twajua mahitaji yetu
Hatupangiwi na mtu.
Eti! Beberu ajigamba
Kujifanya yeye mwamba
Ataka tupanda vichwani
Kwa nchi hatuna utani
Hatutaki udhalimu
Chambilecho Mwalimu.
“Linalia la mgambo
Lisikike mpaka ng’ambo:
Tumechoka kuonewa!
Tumechoka kuchezewa!
Tuseme: sasa basi
Ubeberu na uasi”.
Vijana Tazania
Wote shime kwa nia
Jitihada na maarifa
Tulitete letu Taifa
Adui asipate mwanya
Kutufinyanga kama nyaya.
Kifika Oktoba ishirini na nane
Kwa dhati tushikamane
Jambo letu twalijua
Kuiheshimisha Tanzania
Beberu akome akomae
Kama corona, asituzoee.
Beberu ni joka hatari
Tulipondeponde kwa ari
Nia ya kizalendo tunayo
Uwezo na nguvu tunavyo
Sababu pia zinatosha
Kunyonywa imetosha.
Anao vibaraka wake
Wana hulka kama yake
Twawajua kwa majina
Nao wanataka dhamana
Kuongoza nchi yetu
Kinyume na maslahi yetu.
Wakala wa Beberu
Hatari kuliko Beberu
Nchi yetu twaipenda
Hatuwapi wenye inda
Mola tuepushe na balaa
La wenye kuleta fadhaa.
Tunaye mkombozi wetu
Amesimama kati yetu
Kiongozi makini na safi
Hana suluhu na walafi
Vijana wanamwita baba lao
Anaweka vyema jambo lao.
Ni kamanda wetu mahili
John Pombe Magufuli!
Shime Watanzania wote
Siku ile twende wote
Tukachukue na kuweka
Kwa Magufuli wa uhakika.
Tanzania yapendeza
Amani yetu yaangaza
Uhuru wetu twajivunia
Na tisa hamsini metimia
Beberu we situtishe
Utaipata kasheshe.
Wapo wenye inda
Nia yao kulivurunda
Taifa letu imara
Watuletee madhara
Tunasema hatukubali
Tutawafyekelea mbali.
Twatimiza demokrasia
Viongozi kujipatia
Kwa njia za haki na amani
Kupata walokuwa makini
Twajua mahitaji yetu
Hatupangiwi na mtu.
Eti! Beberu ajigamba
Kujifanya yeye mwamba
Ataka tupanda vichwani
Kwa nchi hatuna utani
Hatutaki udhalimu
Chambilecho Mwalimu.
“Linalia la mgambo
Lisikike mpaka ng’ambo:
Tumechoka kuonewa!
Tumechoka kuchezewa!
Tuseme: sasa basi
Ubeberu na uasi”.
Vijana Tazania
Wote shime kwa nia
Jitihada na maarifa
Tulitete letu Taifa
Adui asipate mwanya
Kutufinyanga kama nyaya.
Kifika Oktoba ishirini na nane
Kwa dhati tushikamane
Jambo letu twalijua
Kuiheshimisha Tanzania
Beberu akome akomae
Kama corona, asituzoee.
Beberu ni joka hatari
Tulipondeponde kwa ari
Nia ya kizalendo tunayo
Uwezo na nguvu tunavyo
Sababu pia zinatosha
Kunyonywa imetosha.
Anao vibaraka wake
Wana hulka kama yake
Twawajua kwa majina
Nao wanataka dhamana
Kuongoza nchi yetu
Kinyume na maslahi yetu.
Wakala wa Beberu
Hatari kuliko Beberu
Nchi yetu twaipenda
Hatuwapi wenye inda
Mola tuepushe na balaa
La wenye kuleta fadhaa.
Tunaye mkombozi wetu
Amesimama kati yetu
Kiongozi makini na safi
Hana suluhu na walafi
Vijana wanamwita baba lao
Anaweka vyema jambo lao.
Ni kamanda wetu mahili
John Pombe Magufuli!
Shime Watanzania wote
Siku ile twende wote
Tukachukue na kuweka
Kwa Magufuli wa uhakika.