USHAIRI

USHAIRI

ramadhani kimweri

Senior Member
Joined
Apr 22, 2016
Posts
181
Reaction score
179
SHAURI YAO
Watasema kila leo, kuwambia walimwengu
Wachapishe matoleo, ya kireno na kizungu
Nimejaliwa upeo, na kisha ninaye Mungu
Hayo wanayo yatenda, yatawarudia wao

Wenda wakidanganyana, kunitangaza ubaya
Kunifanyia khiyana, na maovu kama haya
Mola aweke bayana, mwisho wataona haya
Hayo wanayo yatenda, na yatawadhuru wao

Ni shauri yao hiyo, hayo wanayoyatenda
Machafu wayafanyayo, Mungu ndio hunilinda
Si mazuri wasemayo, husema nisoyatenda
Hayo wanayo yatenda, yatawarudia wao.

Maneno yaso kikomo, mara lile mara hili
Wasema bila kipimo, maneno yaso ya kweli
Waache wapige domo, mimi ninaye Jalali
Hayo wanayo yatenda, na yatawadhuru wao.

kitambo wanitafuta, kutaka tuumbuane
Mimi sitowatafuta, Waache wadanganyane
Tena hawatonipata, wakatafute mwingine
Hayo wanayo yatenda, yatawarudia wao.

Napambana peke yangu, wanangu wale washibe
Kipi mnataka kwangu, mgongoni niwabebe
Kimbilio langu Mungu, mkijifanya wababe
Hayo wanayo yatenda, yatawarudia wao..

[emoji2398]Ibn kimweri.
 
Back
Top Bottom