Ushamba wa kutapika kwenye gari ulivyoniponza

Ushamba wa kutapika kwenye gari ulivyoniponza

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Nikiri tu yakuwa miaka mingi iliyopita mimi nilikuwa mshamba sana wa magari kuazia gari moshi na mabasi ya mikoani.

Siku moja nasafiri kutoka Arusha kuja Dar na basi maarufu sana kipindi hicho Buffalo nilibahatika kukaa karibu na mtoto mmoja matata sana kipindi hicho nilikuwa na kati ya miaka 20 to 22 kutokana na muonekano wangu very handsome by then bishoo haswa mtu asingeweza kunidhania kuwa natapika sana kwenye gari.

Yule binti akaanza kuniongelesha mimi nilikuwa namjibu tu very short coz sikupenda mazoea naye mana angenizoea huenda angenicheka!

Nikavumilia kutapika kishenzi kutoka Arusha mjini to Boma ng'ombe nikaanza kuhisi kichefuchefu hatari na kuanza kujizui ebwana nikajizuia nikaona nakosa pumzi mana nikiangalia ni mm tu gari zima natapika aisee nilijiona mdhaifu sana.

Kwakuwa yule mrembo alikaa upande wa dirishani ikabidi nijikaze nimwambie najisikia vibaya niombe nikae dirishani but kabla ya hayo ilibidi nimpange yakuwa ninaumwa malaria kali sana ili asinione mshamba, nikajiongelesha kwa sauti "Hii malaria isiponiua basi itanikomaza kiaskari🤣[emoji28]" aaah wapi siumwi malaria wala nini ni ushamba tu natapika tena gari ikirudi riverse au ikiwa silencer ndio kabisa.

Baada ya hapo akaniambia "pole but vp umepima"? Nikamjibu ndio na ndio maana naenda Dar kwa mzee kutibiwa akasema poa ebwana kipindi hicho simu ilikuwa kumiliki ni mtiti uwe tajiri au mtoto watajiri la sivyo ningechukua namba ya yule binti alivyokuwa mkarimu.

Wakati sasa ananipisha niende upande wa dirishani nikajizuia kutampika nikamtapikia kuanzia kifuani mpaka mapajani tena tapiko lenye harufu kali kweli but hakujali akatoa khanga na kujifuta akanifuta na mimi tukaendelea na safari aisee.

Niliona aibu sana mana mtoto wa watu alikuwa msafi sana ilibidi gari zima watu waniangalie aisee yani namna nilivyokuwa nateseka nikisafiri nilikuwaga naona safari ndefu kama kifo ila nikipanda hiace au tax nilikuwa sitapiki sijui kwanini.

Baada ya kuzoea safari hizo nenda rudi nenda rudi hatimaye ushamba ule uliniisha nikawa naipebda sana safari ndefu.
 
Bora wewe ulikuwa tapika tapika unatembea na mfuko wa malboro/rambo...

Sasa kuna wale mabingwa wa kubanwa haja kubwa, yaani wao wakiwa safarini matako yao lazima yaingiwe na kiherere cha kuharisha...

Kuna binti mmoja wakati fulani naenda Kigoma, alimanusura aharishe kwenye basi, maana si kuhaha kule jasho kila mahali utadhani alilishwa mlenda wenye pilipili...

Basi ilivyotokea tu upenyo basi limesimama sijui ilikuwa Itigi pale, basi binti alitoka mbio nje ka Usain Bolt bila hata kuomba ruksa kwa wale makondakta, maana muda wa volkano kulipuka ulikuwa umetaradadi...
 
Bora wewe ulikuwa tapika tapika unatembea na mfuko wa malboro/rambo...

Sasa kuna wale mabingwa wa kubanwa haja kubwa, yaani wao wakiwa safarini matako yao lazima yaingiwe na kiherere cha kuharisha...

Kuna binti mmoja wakati fulani naenda Kigoma, alimanusura aharishe kwenye behewa, maana si kuhaha kule jasho kila mahali utadhani alilishwa mlenda wenye pilipili...

Mkuu kwani mabasi ya kigoma siku hizi yana mabehewa?
Au ndio tupo chitchat?
 
Mara behewa mara basi... Acha urongo
Bora wewe ulikuwa tapika tapika unatembea na mfuko wa malboro/rambo...

Sasa kuna wale mabingwa wa kubanwa haja kubwa, yaani wao wakiwa safarini matako yao lazima yaingiwe na kiherere cha kuharisha...

Kuna binti mmoja wakati fulani naenda Kigoma, alimanusura aharishe kwenye behewa, maana si kuhaha kule jasho kila mahali utadhani alilishwa mlenda wenye pilipili...

Basi ilivyotokea tu upenyo basi limesimama sijui ilikuwa Itigi pale, basi binti alitoka mbio nje ka Usain Bolt bila hata kuomba ruksa kwa wale makondakta, maana muda wa volkano kulipuka ulikuwa umetaradadi...
 
Mimi pia nilikuwa natapika, hadi leo nisipokaa vizuri natapika mfano nikijiroga ninywe maji asubuhi asubuhi tayari, kiukweli nimeteseka sana na hili tatizo
 
Hii kutapika kwenye mabasi si ushamba ni kama niseme allergy ndio maana hata wamiliki baadhi wa vyombo vya mafuta vya kusafiria wanagawa mifuko ya plastiki au mifuko ya karatasi ngumu
 
Mimi pia nilikuwa natapika, hadi leo nisipokaa vizuri natapika mfano nikijiroga ninywe maji asubuhi asubuhi tayari, kiukweli nimeteseka sana na hili tatizo
Pole sana kuwa na mazoea ya kusafiri mara kwa mara itakata na pia ukisafiri usikae nyuma kaa karibu na dereva mitikisiko na mizunguko ya gari inakuwa sio mikubwa
 
Hii kutapika kwenye mabasi si ushamba ni kama niseme allergy ndio maana hata wamiliki baadhi wa vyombo vya mafuta vya kusafiria wanagawa mifuko ya plastiki au mifuko ya karatasi ngumu

sio allergy kitaalam inaitwa resistance yani akili yako unakataa kuona miti inarudi nyuma, kuona mbali na kukukuta mda huo huo, mitikisiko nk hivyo mwili wako unapinga ndio mana unatapika ukiamini kuwa kuna kjtu umekula/kiko tundoni kinakupa shida
 
Pole sana kuwa na mazoea ya kusafiri mara kwa mara itakata na pia ukisafiri usikae nyuma kaa karibu na dereva mitikisiko na mizunguko ya gari inakuwa sio mikubaa
Ndugu nitasafiri mara kwa mara bila sababu? Ila nna miaka karibu nane sijatapika sijajua ile hali imetoka au ni kwa sababu huwa nachukua tahadhari sana. Ila nadhani inatokea tu kusafiri mara nyingi sio sababu maana kuna wengine huwa hawasafiri sana ila hawatapiki ng'oo
 
Mm ndio tatizo langu kubwa kutapika kwenye mabasi huwa na beba mifuko kabisa

Pole sana ukiingia ktk gari relax na uamini upo sehemu sawa na uliyoizoea, pili penda kusafiri mara kwa mara hata safari fupi fupi usingoje mwaka ndio usafir, tatu kaa siti mbele usikae nyuma kwani mtikisiko na mzunguko wa gari ni mkubwa ikatwapo kona au kupanda tuta
 
Ndugu nitasafiri mara kwa mara bila sababu? Ila nna miaka karibu nane sijatapika sijajua ile hali imetoka au ni kwa sababu huwa nachukua tahadhari sana. Ila nadhani inatokea tu kusafiri mara nyingi sio sababu maana kuna wengine huwa hawasafiri sana ila hawatapiki ng'oo

Hili tatizo lipo kwenye ubongo ndio mana mwingine akinywa pombe hatapiki mwingine anatapika hivyohivyo kwenye gari tumeumbwa na ubongo tofauti mingine huchukua muda kukubali new situations but mingine ina resist
 
Pole sana ukiingia ktk gari relax na uamini upo sehemu sawa na uliyoizoea, pili penda kusafiri mara kwa mara hata safari fupi fupi usingoje mwaka ndio usafir, tatu kaa siti mbele usikae nyuma kwani mtikisiko na mzunguko wa gari ni mkubwa ikatwapo kona au kupanda tuta
Mimi nnavyopenda siti za nyuma sasa hasa kwenye daladala. Nikiingia yale magari kama yale ya gongolamboto naenda kujichimbia kwenye konaa
 
Back
Top Bottom