Ushamba wa kutapika kwenye gari ulivyoniponza

Ushamba wa kutapika kwenye gari ulivyoniponza

sio allergy kitaalam inaitwa resistance yani akili yako unakataa kuona miti inarudi nyuma, kuona mbali na kukukuta mda huo huo, mitikisiko nk hivyo mwili wako unapinga ndio mana unatapika ukiamini kuwa kuna kjtu umekula/kiko tundoni kinakupa shida
Aaaah
 
Mimi nnavyopenda siti za nyuma sasa hasa kwenye daladala. Nikiingia yale magari kama yale ya gongolamboto naenda kujichimbia kwenye konaa
Mmmmmmmh nyuma sikai labda siti za mbele zijae, mie napenda kukaa mbele kule na dereva
 
Nikiri tu yakuwa miaka mingi iliyopita mimi nilikuwa mshamba sana wa magari kuazia gari moshi na mabasi ya mikoani.

Siku moja nasafiri kutoka Arusha kuja Dar na basi maarufu sana kipindi hicho Buffalo nilibahatika kukaa karibu na mtoto mmoja matata sana kipindi hicho nilikuwa na kati ya miaka 20 to 22 kutokana na muonekano wangu very handsome by then bishoo haswa mtu asingeweza kunidhania kuwa natapika sana kwenye gari.

Yule binti akaanza kuniongelesha mimi nilikuwa namjibu tu very short coz sikupenda mazoea naye mana angenizoea huenda angenicheka!

Nikavumilia kutapika kishenzi kutoka Arusha mjini to Boma ng'ombe nikaanza kuhisi kichefuchefu hatari na kuanza kujizui ebwana nikajizuia nikaona nakosa pumzi mana nikiangalia ni mm tu gari zima natapika aisee nilijiona mdhaifu sana.

Kwakuwa yule mrembo alikaa upande wa dirishani ikabidi nijikaze nimwambie najisikia vibaya niombe nikae dirishani but kabla ya hayo ilibidi nimpange yakuwa ninaumwa malaria kali sana ili asinione mshamba, nikajiongelesha kwa sauti "Hii malaria isiponiua basi itanikomaza kiaskari🤣[emoji28]" aaah wapi siumwi malaria wala nini ni ushamba tu natapika tena gari ikirudi riverse au ikiwa silencer ndio kabisa.

Baada ya hapo akaniambia "pole but vp umepima"? Nikamjibu ndio na ndio maana naenda Dar kwa mzee kutibiwa akasema poa ebwana kipindi hicho simu ilikuwa kumiliki ni mtiti uwe tajiri au mtoto watajiri la sivyo ningechukua namba ya yule binti alivyokuwa mkarimu.

Wakati sasa ananipisha niende upande wa dirishani nikajizuia kutampika nikamtapikia kuanzia kifuani mpaka mapajani tena tapiko lenye harufu kali kweli but hakujali akatoa khanga na kujifuta akanifuta na mimi tukaendelea na safari aisee.

Niliona aibu sana mana mtoto wa watu alikuwa msafi sana ilibidi gari zima watu waniangalie aisee yani namna nilivyokuwa nateseka nikisafiri nilikuwaga naona safari ndefu kama kifo ila nikipanda hiace au tax nilikuwa sitapiki sijui kwanini.

Baada ya kuzoea safari hizo nenda rudi nenda rudi hatimaye ushamba ule uliniisha nikawa naipebda sana safari ndefu.
sio wewe tu hata bashite ana tatizo kama hilo ila yeye anatapikaga kwenye ndege
 
Kutapika ni ushamba?
Wengi wanachukulia hivyo. Kuna kipindi tuliendaga tour, mimi nilitapika wakati wa kwenda. Siku moja darasani kukawa na argument na mkaka mmoja alipozidiwa akaniambia utaniambia nini we mshamba unayetapika kwenye magari. Kwa kweli nilijisikia vibaya, nilimchukia, alipofeli mtihani wa form two nilifurahi kishenzi
 
Mkuu ungepanda boti nadhani ungefariki kabisa
Siku ya kwanza kukatiza bahari nilijikanyaga nikapanda boti ya uvuvi

Nilijua ndiyo siku ya mwisho wa maisha yangu ilikuwa ni jioni na bahari ilikuwa chafu yani mawimbi ya kutosha yani katika safari yote boti inaenda kama inapanda vilima na kushuka
Hali kama hiyo inafanya unaona kama vile tunazama kumbe hatuzami, kama tunazama kumbe hatuzami kama tunazama kumbe hatuzami yani ndiyo safari hiyo yote ni kama uko mahali na Mtu anatishia kukubwaga vile
Sasa hofu yake siyo ya kawaida mwili wote unaishiwa nguvu hata kusimama tu huwezi unakuwa mgonjwa mahututi kutapika kwingiii
unakuta masela wako pale mbele kabisa stori nyingi bangi zinatembea tu hawana habari
Sometime wimbi linazidi maji yanachapa boti yanaingia ndani
Nikiri tu yakuwa miaka mingi iliyopita mimi nilikuwa mshamba sana wa magari kuazia gari moshi na mabasi ya mikoani.

Siku moja nasafiri kutoka Arusha kuja Dar na basi maarufu sana kipindi hicho Buffalo nilibahatika kukaa karibu na mtoto mmoja matata sana kipindi hicho nilikuwa na kati ya miaka 20 to 22 kutokana na muonekano wangu very handsome by then bishoo haswa mtu asingeweza kunidhania kuwa natapika sana kwenye gari.

Yule binti akaanza kuniongelesha mimi nilikuwa namjibu tu very short coz sikupenda mazoea naye mana angenizoea huenda angenicheka!

Nikavumilia kutapika kishenzi kutoka Arusha mjini to Boma ng'ombe nikaanza kuhisi kichefuchefu hatari na kuanza kujizui ebwana nikajizuia nikaona nakosa pumzi mana nikiangalia ni mm tu gari zima natapika aisee nilijiona mdhaifu sana.

Kwakuwa yule mrembo alikaa upande wa dirishani ikabidi nijikaze nimwambie najisikia vibaya niombe nikae dirishani but kabla ya hayo ilibidi nimpange yakuwa ninaumwa malaria kali sana ili asinione mshamba, nikajiongelesha kwa sauti "Hii malaria isiponiua basi itanikomaza kiaskari[emoji1787][emoji28]" aaah wapi siumwi malaria wala nini ni ushamba tu natapika tena gari ikirudi riverse au ikiwa silencer ndio kabisa.

Baada ya hapo akaniambia "pole but vp umepima"? Nikamjibu ndio na ndio maana naenda Dar kwa mzee kutibiwa akasema poa ebwana kipindi hicho simu ilikuwa kumiliki ni mtiti uwe tajiri au mtoto watajiri la sivyo ningechukua namba ya yule binti alivyokuwa mkarimu.

Wakati sasa ananipisha niende upande wa dirishani nikajizuia kutampika nikamtapikia kuanzia kifuani mpaka mapajani tena tapiko lenye harufu kali kweli but hakujali akatoa khanga na kujifuta akanifuta na mimi tukaendelea na safari aisee.

Niliona aibu sana mana mtoto wa watu alikuwa msafi sana ilibidi gari zima watu waniangalie aisee yani namna nilivyokuwa nateseka nikisafiri nilikuwaga naona safari ndefu kama kifo ila nikipanda hiace au tax nilikuwa sitapiki sijui kwanini.

Baada ya kuzoea safari hizo nenda rudi nenda rudi hatimaye ushamba ule uliniisha nikawa naipebda sana safari ndefu.
 
Pole sana kuwa na mazoea ya kusafiri mara kwa mara itakata na pia ukisafiri usikae nyuma kaa karibu na dereva mitikisiko na mizunguko ya gari inakuwa sio mikubwa
Awe na mazoea ya kusafiri hata kama hana sababu ya kumfanya asafiri..!![emoji3]
 
Daaah!me masuala ya kutapika safarini cnaga hayo mambishe kabisa. Labda chalii yangu ni akila vitu vyenye mafuta mingi ndo anatapikaga kwa road.but mm hata unilishe kiporo cha makande hiyo morniee halafu nipakie fuso uniweke kwenye kabichi huko nyuma.asee!kutapika labda yesu arudi.🏃🏃🏃🏃🏃
 
Mkuu hiyo yako ndogo mbona!
siku moja jioni pale ubungo kuna jamaa alikua kajaza watu kumbe ni wale wanaouza madawa huku wanaonehsa viexperiment vyao vya uongo na ukweli ili kukamata watu. Sasa akawa anauza dawa ya kusafisha tumbo mzee baba nikachukua. Asubuhi na mapema nikamix packet yote kwenye supu nikagonga kiulaini. Nikaenda kupanda bus kuelekea iringa. Sasa ile nafika mbezi nikaanza kuhisi valve zinataka kublow down ila nikajikaza ebwaana eeh kufika maili moja sasa...... sitakuja kusahau.
 
Ulikosea mkuu dawa za kusafisha tumbo unapaswa uwe off nyumbani
 
Basi mkuu, nilighafilika wakati wa kuandika nilijisahau nikaandika behewa kwa mazoea ya usafiri maarufu wa Kigoma
Hivi lilikuwa basi au treni[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom