Ushamba wa TRA unatuumiza wananchi

Ushamba wa TRA unatuumiza wananchi

Gulwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2008
Posts
10,597
Reaction score
16,394
Jana niliishiwana umeme nyumbani kwangu. Kila nikijaribu kununua kwa simu kama nilivyosmzoea ilishindikana.

Leo nikaamua kwenda TANESCO kuulizia tatizo ni nini. Baada ya kuwapa namba ya mita yangu nikaambiwa kuwa sababu nyumba ni ya ghorofa natakiwa kulipia elfu tano kwa kila floor na deni linatakiwa kulipwa tangu 2022 mpaka sasa ndio nipate kuuziwa umeme kama kawaida.

Swali ni nalijiuliza ni je kujenga ghorofa ni ishara ya kuwa na pesa nyingi bila kujali ukubwa wa eneo la nyumba? Zipo nyumba nyingi sana zisizo za ghorofa zenye thamani kubwa kuliko ghorofa.

Hii inadhihirisha kuwa tuna wasomi wasiotumia vichwa vyao vizuri na wanaishi kwa kukariri tu.

Kinachonisikitisha ni kuwa utaratibu huu wa kutufungia tusipate umeme haukutangazwa rasmi
tukajiandaa bali tumeshtukizwa.

Kweli waendelee kuupiga mwingi na kutukamua ili waendeshe maisha ya anasa kwao na familia zao ila ipo siku haki itatatawala
 
Hongera mkurugenzi kwa kumilii nyumba ya ndoto yangu.
 
Back
Top Bottom