Hata humu ndani ya JF kuna watu tunaweza kuwaita Ma-vuvuzela a.k.a Lepatata.Nasikia wale waliomo ndani ya mahusiano ambao wana irritating noises kwa wale wawapendao tayari wameshaanza kuitwa vuvuzela.
we acha tu wasouth wana nongwa alafu hawa wenye rangi yetu ni wabaguzi kupita kiasi.Inaboa kwa kweli hasa ukiwa nao live uwanjani, mechi yao vs Mexico sikufaidi hata wengine walikuwa bize kupiga vuvuzela kuliko kuangalia mechi, yani waliposawazisha Mexico ikawa utulivu kidogo.
Yani wengi watalalamika mwaka huu inaboa vuvuzela inaumiza masikio, Blatter kamuheshimu Mandela na anawajua angekataza wangegoma kuja uwanjani, mana weusi wa bondeni siasa zimewajaa sana kiasi wanaona kila kitu wao ndio wapo sawa.
Noja wakitoka utaona peupe, mana wapo radhi waone marudio isidingo na generation kuliko Brazil vs Ureno live, kuna sehemu wanaonyesha public lakini wanafungua na kujaa siku Bafanabafana ikicheza tu, wakitolewa viwanja vitakuwa vyeupe.
Ni ulimbukeni na wengi ni sifa tu kushindana kuyapiga, si unajua sifa za kijinga
Hizi ni Vuvuzela au Vuvudzela?
vuvuzela ni mwisho wa matatizo.
Wafaransa wameshapata kisingizio cha kwa nini hawawezi kushinda. Brazil, argentina na german hazikuwasumbua kabisa na wakashinda.
Yanaudhi kweli ila kwa sasa yamekuwa kama tondo tundu. Wc ikiisha, wengi watayakumbuka.
Haijalishi ili mradi inasomeka inatamkika vuvuzela.Hizi ni Vuvuzela au Vuvudzela?
Naona Vuvuzela zimeshapamba moto, Wafaransa mbona leo sura zao zimekuwa ndefu ....mida mida kipute kinaanza. Nilifikiri Ze Bluez wataweka mpira kwapani lakini nawaona kwenye tunnel.