Usharuri inahitajika: Kati ya MD na Dental surgery kozi ipi asome

Hapa hatuongelei US, tupo Bongo kaa kwa kutulia andika tena.
 
Guys , nimesoma ushauri wenu nimeelewa lakini naona uzito umebalance, Samahanini wakuu kwa usumbufu lakini Kama Kuna mtu ana uzoefu na Kati ya Kozi moja aniambie nichukue hiyo mimi
 
Nenda kasome DDS. Market yake ni kubwa na haichuji. Kila mwaka nafasi za hawa mabwana hua zinakua readvertised. Itachukua muda mrefu sana hadi hii course iwe saturated. Na kama unavyojua, DDS iko Muhimbili only na labda waliosoma nje.

On the other hand, MUHAS, KCMC, UDSM, CUHAS, KIUT, IFAKARA etc etc wote wanamwaga madaktari mtaani.

It’s also easy kujiajiri kama dentist tofauti na MD ambayo inabidi muwe wengi cause polyclinic inahitaji mtaji mkubwa kidogo.

Kasome DDS, MD waachie wenye wanajua watakapoenda baada ya shule.
 
Asante sana kwa ushauri wako mkuu
 
Hii inakuwa kama kusomea procurement. Miaka mitatu unasomea kununua, kweli?
 
Siyo jino tu. Ni meno 32 ya MTU mzima na meno 20 ya mtoto na kinywa kwa ujumla. Ndo maana ana itwa Daktari ya kinywa na meno. Na siyo jino.

Meno hayana tofauti ni yale yale kimuundo,kwahiyo ukiamua hata kuyasoma yote miaka miwili mingi sana,miaka 6 nimupoteza muda tu nadhani hua mnarudia mana yakusoma vinaisha.
 
Unachokiongea hukijui
 
Mnaongea ujinga gani nyie
 
Dentist sio daktari hana hadhi wala sifa ya kuwa daktari labda awe dokita manyaunyau.

Narudia tena MD inasoko sana maeneo mengi ya kufanyia kazi.
Yesu wangu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]mimi nipo hapa muhimbili Unachoongea hukifahamu wewe !nyie ndo mnapoteza vijana
 
Meno hayana tofauti ni yale yale kimuundo,kwahiyo ukiamua hata kuyasoma yote miaka miwili mingi sana,miaka 6 nimupoteza muda tu nadhani hua mnarudia mana yakusoma vinaisha.
Unaongea kwa kuhisi au unafahamu !wewe jamaaa unaongea vitu uvijui usichukulie viti simple hvyo !wamekaaa maprofessor wameona iwekwe miaka mitano Sjui unaongea nini!Udaktari wa Meno ni Specialization , mwaka wa kwanza mpaka wa tatu MD na DDs wanasoma vitu Vyote sawa then miaka inayobaki wanaenda tofauti ! Udaktari wa meno una Ajira nzuri sababu wanaomaliza ni wachache !wewe unachukulia kwamba DDS wanasoma tu kuhusu Jino kumbe wanasoma kwanzia kwenye meno mpaka Kifuani , Magonjwa yote yanayohusu na namna yakudeal nayo pamoja na upasuaji wa magonjwa kama cleft na vitu vingine kibao! Kama hufahamu kitu Uliza maana unapotumia akili ya unachokizania utaarifu Future ya watu! MD ilikuwa na soko zamani kipindi wataalamu ni wachache hvyo MD alikuwa anauza hadi dawa yeye ndo Mtaalamu wa meno pia ila sasa hivi Wametolewa kazi ya dawa Na mtaalamu ni Mfamasia (ambayo nasoma mimi hapa Muhimbili) na kinywa ni Dental.
 
Meno hayana tofauti ni yale yale kimuundo,kwahiyo ukiamua hata kuyasoma yote miaka miwili mingi sana,miaka 6 nimupoteza muda tu nadhani hua mnarudia mana yakusoma vinaisha.
Kwa akili zako unadhani wanaanza kusoma jino day one [emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Kozi zote za afya ngazi ya degree za miaka 4/5 mnaanza kubobea kwenye fani husika kuanzia mwaka wa 3. Miaka 2 ya mwanzo ni kusoma mwili wote upoje na unafanyaje kazi.

Huwezi kusoma jino tuu bila kujua mzunguko wa damu upoje, you treat the patient as whole sio system moja tuu. Mambo huwa yanaingiliana lazima usome vyote ndio ubobee kwenye kipande chako.
 
Dental watu wana underate ila ina maisha sana kwa sasa kuliko MD ni vile tu vijana wengi hatufanyi research tumekariri.

Kwasasa kozi za afya angalau hazina njaa.

Radiology
Dental
Optimetry
Physiotherapy
MD(hii now imepungua thamani kutokana na utitiri wa MD& CO mtaani kwani kila mtu anataka kua daktari wa kutibu magonjwa).

Ukipata nafasi kwenye 3 za juu kimbilia haraka.,mtaani hela ipo.
 
Dentist sio daktari hana hadhi wala sifa ya kuwa daktari labda awe dokita manyaunyau.

Narudia tena MD inasoko sana maeneo mengi ya kufanyia kazi.
Upotoshaji mkuu huu,,nimesoma MD mimi hao dentist tumesoma nao na mtihani ni mmoja tulikua tunapewa saa ingine anakuzid wewe MD,,kuanzia mwaka wa 3 wanakua idarani kwao
 
Clinical officer
Miaka mitano plus 1 wa mafunzo unasomea jino eti jino,tuweni serious hiyo kozi miaka miwili inatosha kabisa kuisoma,Udaktari unahishima yake na sifa kwa watu wa MD au VM.
Fanya tafiti ya unachokisema kuhusu DDS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…