Ushauli wangu kwa serikali yetu

Ushauli wangu kwa serikali yetu

D2050

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
1,919
Reaction score
1,094
Hali ya upatikanaji wa mitaji ya biashara kwasasa hapa nchini ni mbaya sana hususani kwa wafanyabiashara wadogo wadogo,
Serikali inapaswa kuangalia namna ya kuwekeza ktk mikopo ya kibiashara kiurahisi kwa mitaji midogo midogo.
Hakuna benki ambayo inaweza kumwamini mtu ikampa mkopo wa 1,000,000 bila kuweka zamana ya kiwanja.taasisi iliyokuwa inauwezo wa kukopesha bila zamana ya nyumba ni PRIDE pekee

Ushauli wangu kwa serikali kama mnania ya kweli kuinuwa mitaji ya wafanyabiashara wadogo wadogo nendeni mkachukue orodha ya wateja wa pride Tanzania na taratibu zao walivyokuwa wanaendesha shirika lao ziboresheni anzisheni taasisi ya kifeza ambayoitakuwa rafiki kwa wakopaji.

PRIDE imefilisika lakini iliweza kuwekeza seven kubwa sana hapa tz pamoja na mapungufu yake itabaki kuwa taasisi iliyowainua watu wengi.

Finka wanajaribu kuwekeza na wao lakini ribs ya mikopo yao haiko rafiki sana kwa mkopaji.
Benki ya wanawake mikopo yao ilikuwa mizuri lakini watendaji wao wameshindwa kuwa wafuatiliaji wazuri wa mikopo wanayoitoa kwa wakopaji wao hawana mda nao watakuwa kama pride watafilisika.
Serikali wekezeni kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ili kuinuwa uchumi wa wataifa
 
Back
Top Bottom