Tanzania kuna watoto wengi sana wanaingia shule kwa kasi kuliko uwezo wa serikali kuajiri walimu wa kutosha. Huu ni wakati mzuri wa kufikiria programu ya wahitimu wa elimu za juu ambao wengi nao ni vijana kufundisha kwenye shule mbalimbali kwa mwaka.
Serikali iweke utaratibu mzuri hili linawezekana kukabiliana na tatizo kubwa la walimu. Mpango huu uwe wa mpito na uwe wa kujitolea kwa masharti mazuri. Haya ni mambo ambayo napendekeza:
Serikali iweke utaratibu mzuri hili linawezekana kukabiliana na tatizo kubwa la walimu. Mpango huu uwe wa mpito na uwe wa kujitolea kwa masharti mazuri. Haya ni mambo ambayo napendekeza:
- Wanavyuo akijitolea kufundishwa asemehewe mkopo wake wa elimu kwa asilimia 30% kwa mwaka. Mfano kama deni lako ni Tsh 12M basi msamaha kwa mwaka ni Tsh 4M.
- Kuwe na program za kuwaandaa kwa muda wa miezi miwili kabla ya kuondoka chuo.
- Kwa wale watakaofanya vizuri kwenye hii program na kuonyesha matokeo, mkataba unaweza kuongezwa kwa mwaka mmoja. Lakini hii program isizidi miaka miwili.
- Wahitimu wa sayansi na teknolojia wapewe kipaumbele.
- Hii program iwe ya kizalendo zaidi kama ilivyo JKT
- Shule za vijijini zipewe kipaumbele zaidi