Ushauri: Azam Media unganeni na Canal Sports mrushe EPL kuleta ushindani

Mwl Athumani Ramadhani

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
1,280
Reaction score
2,522
Kama azam ikaingia UBIA na canal Sports KWA baadhi ya Chanel's za mpira wa ulaya itapata soko zaidi kuliko sasa.

Kwa soko la Tanzania DStv inawaumiza wapenzi wa soka KWA gharama kubwa Sana hivyo inapaswa ipewe ushindani Ili wananchi wapate huduma Bora.

Azam wanaweza pandisha vifurushi hadi kufika 40000/= KWA mwezi KWA wale wanaotaka ku access Chanel's za epl za canal Sports! Na hiyo ikasaidia wapenzi kulipa KWA urahisi kuliko Sasa hivi ambapo tunalipa 56000/=,91000/=,81000 na 28000/= KWA DStv nchini!

Meneja masoko wa Azam mnaweza mkafikiria hilo KWA msimu ujao au huu unaoendelea na mkapiga pesa coz wapenzi wa soka la bongo tupo sana nchini!

Nawatakia KILA la kheri katika utekelezaji wenu!
 
Unashindwaje kujua kuhusu mkataba wa haki za matangazo ya EPL
Inawezekana we jamaa!kwani kampuni mbili haziwezi ingia mkataba juu ya chanel fulani!!?
Halafu gharama hazipo constant ujue mbona hao canals wapo chini kuliko DStv!!?

INAWEZEKANA KWA MFUMO HUU HAPA;-

EPL INAINGIA mkataba na canal Sports then canal INAINGIA mkataba na Azam media kufidia gharama na ushindani kibiashara!

Simple tu
 
Haiwezekani kwakuwa Canal amepewa haki kurusha matangazo maeneo wanayozungumza Kifaransa tu.

Hizi Canal tunazotumia si unajua tunaibia kutoka kwa ndugu zetu wa Rwanda, Burundi na Congo!
Wakomae tu kwani supersport kwanini bei zao zinatofautiana eneo la maziwa makuu,yaani gharama vifurushi zinatofautiana kenya,Uganda na Tanzania wakati huduma ni zile zile !wanatufanya mazuzu!
 
Hii issue huwa naona inaweza kuwa na mlolongo mrefu zaidi ya tudhaniavyo..

Kuanzia kwa Barclays, uje DSTV, uteremke Canal Sports mpaka uifikie Azam[emoji848][emoji848]

Inawezekana jamaa wanajua, kufanya hivyo wataharibu brand ya ligi pendwa ya Uingereza, ndio maana wanaacha kwa wachache.
 
Hawa canal hawapo kisheria huku Mzee watu wanaingia kijanja tu, hii ishu sa ivi inawaletea shida sana jamaa wa vibanda umiza, Tanzania hapa DStv tu ndo ana sole right ya epl hizo zingine ni janja janja
 
Nini unajua kuhusu Premier League Production??..PLTV
 
Sio biashara ya uchuuzi kwamba Kuna wholesale - retail- mpaka kumfikia mteja.

Huwezi kuchukua haki ya kurusha mechi za epl kwa canal hata siku moja...Nenda kwa jamaa wanaohusika moja kwa moja
 
Muwekee na gharama za hizo TV rights halafu alone kama Azam anaweza kumtoa dstv
 
Ushaambiwa epl kashamuuzia skyports na bt kwa billions ya ££, yaani tzs trillion kadhaa. Katika mikataba yao wameziba hio mianya unayofikiria. Sky na bt wanauza kwa watu kama dstv na dstv wakati ananunua anaweka mikataba ya kumlinda.
 
£2B
 
Hii taarifa sio sahihi mkuu.

1. Dstv anakaa meza Moja na Epl


Ushahidi huo hapo Dstv analipia mpunga mwingi sana EPL direct.

2. Canal Sport ni Chanel ya Ufaransa ambayo inamilikiwa na Vivendi, ni likampuni kubwa sana Asset zake tu zinafika Trilioni 100 so kusema hawawezi ku Afford hivyo visenti vya Epl ni utani mkuu.

Wewe unachanganya Right za kuonesha EPL Uingereza na za kuonesha Epl nje ya Uingereza.

Uingereza ndio Epl wanaonesha hao kina Sky na BT ukienda Marekani wana NBCSN, Africa kuna DSTV, Bein na Canal, Canada Dazn, Asia ya kusini Super Sport etc.
 

Umeeleweka [emoji1531]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…