Ushauri: Azam Media unganeni na Canal Sports mrushe EPL kuleta ushindani

Dstv amelipa $222M kwa mwaka kununua Epl, mtu yoyote anaweza kumtoa Akibid hela nyingi zaidi, kwa hela zetu ni around bilioni 520

Data za 2021 zinaonesha Azam Vingamuzi vyao havifiki hata Milioni 1, Assume now wamefika hio millioni 1, kurudisha hio hela hawawezi kucharge 40,000.


Canal hawezi muuzia Azam na ni ujinga kibiashara kumuuzia why asije Mwenyewe kuonesha na Kumpiku DSTV amfaidishe Azam.

Niliwahi kuelezea humu kwanini Canal bei zipo chini, unaponunua Epl unalipa Hela fixed, jinsi unavyokuwa na wateja wengi ndio jinsi unavyopata hela nyingi na ndio jinsi unavyocharge hela kidogo.

-Canal plus ana wateja milioni 23 akiicharge 25,000 tu kwa mwezi ana uwezo mzuri wa ku Afford EPL sababu customer base ni kubwa.

-Dstv ana wateja 9m S.A ila wa premium hawafiki hata 2m, overall wanao kama 21m sina data za Africa nzima premium ila ukicheki data za juu hawafiki 5m Africa nzima. Ndio maana unaona kuna vifurushi vinazidi laki.

Hata kidunia sehemu kama India, China, Marekani ni bei rahisi sana Epl sababu wapo wengi, Dazn kama 30,000 tu na peacock (Nbcsn) kama 12,000 tu.
 
Naona ndo hivi pia..

Maana pia mechi za lunchtime jumamosi huko UK huwa hazionyeshwi na hao Sky na hao BT i.e hawana haki nazo..lakini huku Africa tunacheki games zote 360 za PL..
 
Naona ndo hivi pia..

Maana pia mechi za lunchtime jumamosi huko UK huwa hazionyeshwi na hao Sky na hao BT i.e hawana haki nazo..lakini huku Africa tunacheki games zote 360 za PL..
Sasa hivi Overseas Broadcaster wanaingiza Hela nyingi Epl kuliko wale wa ndani, Timu zinapiga mpunga zaidi kuuzia wa nje hakuna sababu kuwapa kina Sky na BT ukiranja wakati wao hawatoi hela nyingi.
 
Ndio maana walimu mnaitwa wapumbavu
Upumbavu wangu ni upi hapo!!?

Kuuliza!!?

Hujui kuwa mi ni mmiliki wa hizo sehemu za Burudani tena nalipia DStv business (81000 kwa 28000) BADO decoder Mbili za Azam 46000/=) piga hesabu sawa na sh ngapi kwa mwezi BADO bills za umeme na kila kitu Sasa kwanini nisiwaze hivyo au UNAFIKIRI Mimi sijaangalia option zote!!?

Mdau kasema hapo juu kuwa haki za kurusha epl DStv wanazipata TOKA kwa BT sport na skysports kama ni Hivyo Basi kwann Azam wasiingie mikataba na canal Sports!!?

Sasa unatoka pooovu au we ni meneja masoko wa DStv!?

KILA la kheri!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…