Ushauri - Azam timueni wachezaji wote

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Sifahamu sheria za soka zinasemaje kuhusu hili , lakini ni wazi kwamba wachezaji wa Azam wanaidhulumu timu yao , hawastahili kufungwa kizembe namna kama wafanyavyo , ni wachezaji wanaopewa karibu kila kitu muhimu kuliko wachezaji wa timu karibu zote za ligi ya Vodacom .

Nini kinachowafanya wafungwe na timu za kuungaunga kama Ndanda na Simba ?

Kuna haja ya uongozi wa timu hii kutafuta watu wengine kabisa , watakaoitumikia timu hii kwa moyo na kwa uaminifu kuliko hawa akina John Boko & co.

Hivi kuna tofauti gani kati ya Azam na TP Mazembe tukilinganisha TREATMENT wanazopewa wachezaji ? Kwanini timu hii inaburuzwa na timu mbovu zisizokuwa hata na posho za uhakika ?

Si bure ! mwanzo nilijua tatizo ni makocha , lakini sasa nimetambua kwamba tatizo kubwa la timu hii ni wachezaji , ambao kuingia kwao Azam ni kama wamemaliza kila kitu , yuko wapi RAMADHANI SINGANO ? Kabweteka baada ya kufanikiwa !
 
Una mawazo kama yangu. Kinachoitafuna Azam kwa sasa ni ile u seniority, kuwaona kina John Boko, Sure boy na wengine, waliopandisha kama ndo wenye team

Azam kwa sasa inabidi kufanya reform kubwa ili kuendana na kasi ya sasa ya soka duniani.. Vinginevyo yatakuwa yale yale tu kila siku. Team ina huduma nzuri ila hakuna kitu.
 
Asante sana mkuu , ifike mahali wachezaji wamuogope Mungu kwa kuwa na uchungu na hela za watu wanaowahudumia .
 
Asante sana mkuu , ifike mahali wachezaji wamuogope Mungu kwa kuwa na uchungu na hela za watu wanaowahudumia .
Suala mkuu sio kwamba hawana uchungu au hawamuogopi Mungu kwa kile wanacho earn dhidi ya return yao.... Ila uwezo wao wachezaji wengi umeshafika kikomo.... Kama makocha wanatimuliwa kwa kukosa mbinu kwa nini na wachezaji wasiondolewe???

Azam watabaki kubadili makocha kila kukicha lakini mchawi wao sio kocha bali wao wenyewe na wachezaji wao. Tazama mtu kama Pep au Moh akiingia sehemu anavyofanya reform.... Sasa Azam kila cku wale wale Hapa Boko, Pale Himid, Huku Sure boy mara Eresto Nyoni...

Hakuna watakachofanya zaidi ya kila siku kuwasindikiza Simba na Yanga... Wakati leo hii tulitaraji Azam iwe TP Mazembe ya East Afrika.
 
Hivi una uhakika hao wachezaji wanapewa kila kitu?

hizi timu zina siri nyiingi sana...usione jina kubwa Azam ukafikiri ni pepo

wafanyakazi tu wa kampuni za Azam wanatia huruma.....

kuna mengi hatuyajui tutakuja kuyajua wakitoka hapo
Mjomba , inawezekana ukawa na hoja , lakini mengine yanaonekana wazi , sijawahi kusikia wachezaji wa azam wamesafirishwa kwa bodaboda au labda kulala gesti yenye kunguni kama timu yetu ya simba kule songea .
 
Azam kuna tatizo
mimi nilipoona siku ile Mrisho Ngasa anaiponda Azam na akarudi Yanga licha ya kutozwa faini
ndo nikajua Azam kuna tatizo kuubwa
 
Bakizeni maneno,msiponde kama Muro wakati mpira unadunda.Kama uwezo wa hao wachezaji umefikia kikomo,kocha ndiye mwenye maamzi.
 
Acha kuiponda timu yangu wewe wanafanya uzembe kivipi we unataka washinde kila siku ili maana ya ushindani isiwepo? Kuna timu gani haipendi kushinda? na hao unaowashauri watimuliwe familia zao utasaidia kulea wewe?
 
Kwamba wamekuja Azam kujikimu siyo ? Wanafungwaje na timu uchwara namna hii aisee ?
 
Bakizeni maneno,msiponde kama Muro wakati mpira unadunda.Kama uwezo wa hao wachezaji umefikia kikomo,kocha ndiye mwenye maamzi.
Wakifanya vizuri tutawasifia lakini kwa sasa tutaendelea kushawishi watimuliwe tu .
 
Kwamba wamekuja Azam kujikimu siyo ? Wanafungwaje na timu uchwara namna hii aisee ?
Kwanza kwenye mpira futa hilo neno timu uchwara,katika mpira kila timu inapambana na inahitaji ushindi..kujikimu ni kwa kila mchezaji awe anatoka nje ya Azam au ndani mana ile ni ajira yao na ni biashara pia
 
Biashara bila faida si itafilisika sasa. Ukiona biashara mbovu si unabadili strategies.
 
Kuna biashara ambayo haina hasara? Hao Azam wamefungwa mara ngapi mpaka wafukuze wachezaji? Je timu kama Yanga ifukuze wachezaji kisa imefungwa na Stendi UTD?
Hatumaanishi kufungwa mechi moja au mbili. Ila return yao ni tofauti na walicho wekeza.
 
Hatumaanishi kufungwa mechi moja au mbili. Ila return yao ni tofauti na walicho wekeza.
Sasa ulitaka wa return kikubwa kivipi? Je Azam wana mtaji mkubwa wa mashabiki
ambao watawaingizia mapato makubwa? Je bidhaa zao wanazouza zinanunuliwa na watu wengi kama zilivyo Simba na Yanga? Timu ndo kwanza inazidi kukua halafu unataka iwe na mafanikio makubwa kwa muda mchache Usiwe mshangiliaji kuwa mshabiki
 
Iv kuna team gani hapa Bongo ina facilities za maana kama Azam. Imefika mpaka wamejengewa viwanja viwili vya mazoezi. Smooth Ground na rough ground, Hostels za wachezaji NK. Kama ni mashabiki huwa wanaruhusiwa kuingia bure Chamanzi pale. Nini tena kinahitajika hapo...
 
Ubishi utakusaidia nini wewe ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…