Ushauri: Baba mkwe katupa kiwanja nijenge na mwanaye wa kike. Ninasita, nikubali au niache sababu naingia mtegoni?

pet geo pet

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2018
Posts
508
Reaction score
788
Wakuu habarini,

Hivi karbuni nimebahatika kufunga ndoa na mke wangu, wakati huo nishampatia mimba.

Hivi karibuni baba mkwe nilimwambia anitaftie kiwanja cha million 1.5 -2, cha kushangaza mzee wa watu akatupa kiwanja cha Bure tujenge mimi na mwanae wa kike, ili hiyo pesa niliyotaka kununulia kiwanja tuweke kwenye ujenzi.

Mpaka sasa hivi nimesita kwanza kujenga hicho kiwanja, ninahofia siku tukikosana au kuachana na mtoto wake itakuwaje na nishajenga nyumba pale?

Wakuu naombeni mnishauri, nijenge au niache kiwanja? Maana kipo katikakati ya mji na amesema tukijenge.

Kuhusu maisha ya baba mkwe yeye yupo vizuri kwani ni msitaafu, hana shida kabisa. Watoto wake karibu wote wapo serikalini.

Ushauri wenu wa muhimu sana, karbuni.
 
Tafuta kiwanja chako, nunua na jenga. Sisi ni binadamu na tunabadilika tabia
Hicho mwachie mkeo.
 
Ushauri wangu kabla ya lolote kwanza HAMISHA UMILIKI WA HICHO KIWANJA TOKA KWA BABA MKWE KUJA KWAKO NA MKEO. Baada ya hapo ndo mambo mengine yaendele kama ni kujenga au kuuza
 
Mwambie No,thanks!

Sio tusi,unamshukuru lakini unakataa.
 
Kwahiyo wakati umemuomba kukutafutia kiwanja haukuona watu wengine mfano madalali? Mambo ya familia yako jitahudi uyapambanie. Baba mkwe wako kakuhurumia ndio maana kakupa kiwanja ili mtoto wake asiteseke. Kuwa na amani!
 
"Watu wema bado wapo"Leejay49
Mkuu nisikilize mimi haya mambo ya kupewa zawadi sijui ya kiwanja au nyumba ina-cost sana

Sawa mtoaji ameona inafaa kutoa but kumbuka ametoa kwa sababu mwanae atalala hapo,lakini baadae itageuka fimbo moja kali sana kwa jamaa pale atakapoambiwa na mkewe “mwanaume gani unaishi ukweni”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…