Ushauri: Baba mkwe katupa kiwanja nijenge na mwanaye wa kike. Ninasita, nikubali au niache sababu naingia mtegoni?

Jenga kwenye hicho kiwanja,halafu nunua kiwanja kingine jenga na baadae nunua kiwanja kingine jenga. Mkikorofishana na mkeo muachie akae na watoto wako hapo.
 
Ushauri wangu kabla ya lolote kwanza HAMISHA UMILIKI WA HICHO KIWANJA TOKA KWA BABA MKWE KUJA KWAKO NA MKEO. Baada ya hapo ndo mambo mengine yaendele kama ni kujenga au kuuza
Yes, anapaswa ahakikishe anafanya UHAMISHO WA MILIKI ya Ardhi hiyo kwanza kabla ya kufanya maendelezo yoyote yale kwenye Ardhi hiyo.

Lazima Ahakikishe kwamba Mkataba wa Mauziano ya Ardhi hiyo (Land Sale Contract) au Hati ya Zawadi (Deed of Gift) inashuhudiwa na Wakili, wasiandikishiane kienyeji. Baada ya hapo anaweza akaendelea kufanya ujenzi kwenye Ardhi hiyo.
 
Pokea hicho kiwanja, then Jenga maisha au Jenga urafiki

Ila usijenge nyumba mkuu... kamwe!
 
Jenga kwenye hicho kiwanja,halafu nunua kiwanja kingine jenga na baadae nunua kiwanja kingine jenga. Mkikorofishana na mkeo muachie akae na watoto wako hapo.
Hii ni nzuri, but believe me hamtodumu kwenye ndoa coz mkigombana kidogo tu utataka umuachie nyumba ukaishi kwenye nyumba yako na uanze maisha yako mengine

Iko hivo, hakuna kitu kinachokosa matumizi mkuu. Hata ukiweka pesa ya emergency basi tegemea emergency lazima itokee ili hiyo hela itumike
 
Bila shaka huku kutakuwa machame au upareni. Mwanangu umeliwa. Hawa wavivu ndivyo walivyo. Nunua chako tena kwenu au mjini unakotaka kuliko kujenga machame au upareni.
 
Akikupa unafata ushauri mnabadili umiliki kuwa wako na mkeo hii inasaidia kuondoa eneo husika kuwa sehemu ya Mali za mkwe ambapo akifariki itabidi igawanywe kwa familia yake
 
Mkuu niliwahi kuuziwa kiwanja kama ulichopewa ww,mfano uniuzie ww uliepewa aisee kidogo kinitoe roho
 
Threads za vijana waliobalehe juzijuzi utazijua tu.
 
Kama wewe ni muhindi/mwarabu ni sawa.

Ila kama sio, achana na hilo suala! Mwanaume unapaswa uwe na vyako akiwemo “mke wako”.

Usijesema hatukukuonya!
 
Kwahiyo wakati umemuomba kukutafutia kiwanja haukuona watu wengine mfano madalali? Mambo ya familia yako jitahudi uyapambanie. Baba mkwe wako kakuhurumia ndio maana kakupa kiwanja ili mtoto wake asiteseke. Kuwa na amani!
Sasa sijui alikuwa anamuambia ili iweje sasa?!
 
Tatizo lako hauji kwenye vikao,
Hili mbona tulisha litolea maamuzi na linasisitizwa kwenye vikao vingi tu.
Acha utolo
 
Huna baba ama ndugu wa kiume ambaye ungeweza kumwomba akutafutie?

Huoni kama ni kutukana ukoo wako?
Mwenyewe imenishangaza sana, kwamba imekuwaje mambo yake binafsi anamshirikisha baba mkwe?

Ndio maana mzee wa watu akaona isiwe tabu, dogo bado hajakomaa ngoja niwape cha bure.
 
Kwahiyo wakati umemuomba kukutafutia kiwanja haukuona watu wengine mfano madalali? Mambo ya familia yako jitahudi uyapambanie. Baba mkwe wako kakuhurumia ndio maana kakupa kiwanja ili mtoto wake asiteseke. Kuwa na amani!
Katika watu woooote kaona mkwe amtafutie kiwanja
Haya mazoea na wakwe sio poa
 
Jenga kwa ajili ya wanao maana hata mkiachana una uhakika kwamba wanao wanapo pa kuishi na wewe utazunguka baadae utarudi hapo hapo maana mnatabia ya kuasi ndoa, mnahangaika na dunia baadae mnarudi kuomba msamaha maisha yanaendea, na kama una uwezo Jenga hiyo baadae Jenga nyingine mbali na pale, ila cha baba mkwe usikiache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…