Ndio Mr. Yebo yebo,
Mimi ni Architect, (Msanifu majengo).
Naomba nami nichangie kidogo.
Kwa mtaji wa 200ml, si mdogo sana itategemea na design ya ramani utakayopendekeza kuchorewa. Hii itategemea aina ya apartment utakoyopendekeza.
ktk jengo hilo hilo unaweza ukaweka apartment za aina tatu tofauti au mbili.
apartment (vyumba 2, kimoja chaweza kuwa na choo, Dining, jiko, sebule , choo na kastoo. )
Mfano kama apartment zina ukubwa wa mita za eneo
40 hadi 80, nikichukua wastani apartment moja itakuwa na
s.q.m 60,
Kwa sasa hapa Dar (Tz) 1 sqm=~350$ , au Tshs. 400,000/= ikiwa ni gharama za materials ,kuchora na wataalamu wote ikimjumlisha pia mjenzi.
Tshs. 400,000x60 sqm = Tshs. 24,000,000mil kwa apartment moja roughly.
Kwa hiyo apartment moja yaweza kugharimu kama 24mil. hivi.
Ktk Mil. 200 /24.0 mil. ~=8
apartment 8, labda tano za 500$ na tatu ni za 600$ rent.
Mwaka wa kwanza utapata kama ifuatavyo
5 apartments x 500$ = 2,500$
3 apartments x 600$ = 1,800$
JUMLA = 4,300$ kwa mwaka wa kwanza
Unaweza kuendeleana Mchanganuo zaidi.
architectmadai@yahoo.com