Ushauri: Biashara ya Apartments Dar es salaam

Ushauri: Biashara ya Apartments Dar es salaam

rafiki you can build the Apartments you want for the 100mil. tafuta mchoro,look for chinese const.firm,wao wataleta vitu from china direct,wanaleta vitu vingi every month for const.projects,watasimamia ujenzi wako within time frame agreed.
vifaa vya ujenzi in Tz vinapandishwa bei na wenye maduka ya hardware,
nakubaliana na wewe. katika construction industry kuna uchakachuaji mkubwa wa bei

yebo yebo
1 bedroom flats zinahitajika sana na unaweza ukazijenga nyingi kwenye eneo lako tafuta tu ramani nzuri

uko uliko ukiangalia 1bed flats ghorofa zinavyobanwa kwenye kiwanja kidogo halafu chini parking utajifunza mambo mengi sana
 
Wadau,

Nafikiria kuingia kwenye biashara ya kujenga na kuzikodisha apartments jijini Dar es salaam.

Nina kiwanja cha 500 sqm maeneo ya katikati ya Morocco na Victoria (upande wa Petrol Station na Knight Support) kama unaelekea Mwenge kupitia New Bagamoyo Road.

Sina uhakika wa soko likoje (scary, I know) ila naona kuna pengo kwenye soko. Walengwa wangi ni vijana wanaopata kazi professional jijini Dar es salaam na wanaotaka kuondoka kuishi na wazazi wao au walitokea mikoani wanaohitaji apartments za kukodisha. Pia nafikiria kulenga wageni wachache wanaokuja Tanzania kwenye kazi za mkataba wa miaka kadhaa.

Lengo langu ni kuwekeza Shs 100 Mil katika kipindi cha miaka 3 ijayo (2012 ujenzi uwe umekamilika). Jengo liwe na apartments 3 au 4 (kutgemea na ushauri wa wachora ramani) kila moja iwe na vyumba 2 vya kulala (1 kiwe ensuite), sebule, jiko, dining, stoo na veranda.

Ili mtaji wangu urudi nategemea nikodishe kila apartment kwa kati 500 – 600 USD kwa mwezi.

Naombeni ushauri wadau, hasa wale ambao pengine tayari wana nyumba za kukodisha Tanzania au wameshajihusisha na mradi kama huu.

Natanguliza shukrani.

Mkuu SS Phares, kama haja yako ni ya kufanya biashara basi utalamba dume.
Kwa eneo hilo unalo litaja kati ya Victoria na Morrocco ni prime area.
Kodi unayoweza kupata kwa apartment hizo ni zaodi ya $500 kwa mwezi, $800-$1000 itategemea finishes za jengo lako.
Ondoa mawazo ya kuwa unataka kuwahudmia watu fulani, sema napangisha fullstop and the market takes over.
Naongea from personal experience.
 
Vipi wote

Kama muanzilishi ya website ya Pango Tanzania nimefanya utafiti kuhusu biashara ya real estate (nyumba viwanja vya kukodisha na kuuza) na nimefikia kwenye conclusion yakua Dar kuna scarcity za nyumba za kukodisha kwa sababu ya wingi wa watu wano hamia dar na nyumba zilizopo sio nzuri sana ndio maana nyumba nyingi mbaya mbaya lakini zina bei kubwa haswa. na madalali wapata pesa kila kukicha kwasababu wanajua watu wengi wanatafuta nyumba.

Wazo lakujenga nyumba zako ni zuri na utapata pesa sana kwanza hapo unapo taka kujenga ni prime kabisa, ila sijui kama Mil 100 itatosha lakini najua utapata nyingi zaidi.

Natafadhali nisaidie kupiga vita hawa madalali kwa ku tangaza nyumba zako katika Pango Tanzania - ni shilingi 15,000 tu hata kama nyumba yako ni millioni 2 wa mwezi au elfu 20 kwa mwezi bei ni hiyo hiyo na silipishi dalali fee ya aina yeyote au komishen yeyote

Jipange uanze you can never go wrong in real estate
 
Ni biashara nzuri lakini 100m bado ni ndogo kwa 3 -4 apartments za vyumba vitatu ...labda uanze na kamoja ........mimi nina appartments maeneo hayohayo ya makumbusho USD 600 kwa mwezi ...nilitumia zaidi ya 350m kwa ajili ya apartments tatu
 
S. S. Phares, wazo safi ila nakushauri utushirikishe na sisi kwa njia ya hisa ili mtaji uwe mkubwa na jengo liwe la kisasa zaidi. Je upo tayari kwa watakao taka kununua hisa?
 
Back
Top Bottom