Ushauri biashara ya kufyatua matofali

hamiii

Member
Joined
Nov 10, 2013
Posts
19
Reaction score
16
Habarini wandugu mie ni mwajiriwa katika taasisi ya kifedha hapa mjini Shinyanga, niko na mwenzangu tumefikiria kuanzia biashara ya matofari kwani ujenzi huku ndio wimbo wa kila mmoja.

Nahitaji kujua vitu vya muhimu sana kwenye hii biashara kwani kwa sasa tumeandaa mtaji wa millioni sita. Ahsanteni.
 
Kitu cha msingi ni kuamua kupata machine either manual ama electricity powered na kupata mtu aliyesome na mwenye uzoefu ili muweze jenga bishala itakayo jiuza, hapa na maanisha tofari zilizo borA , vingine nividogo
 
Tofali za aina gani? Za kuchoma,Saruji au mchanganyiko wa. Saruji na udongo. Siyo fani yangu ila najua baadhi ya aina za tofali
 
Kwa ushauri wangu kwanza utafute yard kubwa ya kutosha yenye uzio (kama utapata) halafu nunua mashine za manual na baadae ya Umeme zipo dar kwa wachina zinafyatua mpaka matofali manne kwa mpigo sio tu matofali kwani baadae ukipata hela unauza na vifaa vya ujenzi pia,
 
Habarini wadau.
Naomba kwa mwenye uelewa wa biashara ya kutengeneza na kuuza matofali ya mchanga ya aina zote kwa ujumla wake anijuze ni vitu gani natakiwa kuwa navyo kwa ajili ya kuweza kufanikisha hili na gharama ya uanzishaji kiwanda cha namna hii kwa mtaji mdogo.

Natanguliza shukrani....
 
Wewe IT Professional, loading error!! syntax error! unataka umuachie nani?
Kabla hujapata huo mchanganuo wa mahitaji! je umesha identify customers wako wanataka nini?
 
Unahitaji vitu hivi
1. Eneo ambalo lipo karibu na barabara
2. Mashine ya kuchanganya mchanga na cement (kuna za umeme n.k)
3. Cement mifuko kadhaa
4. Lori kadhaa za mchanga
5. Vibao vya kuwekea tofali 500 (hv nunua mbao nenda kwa fundi mbao akutengenezee)
6. Tembelea wafanyabiashara wanaouza matofali wakupe data zaidi (Hili ni la msingi zaidi)
7. Utahitaji pia nguvukazi ya vijana angalau 5 (huwa wanalipwa kutokana na mifuko ya cement iliyotengenezwa siku hiyo)
8. Nakutakia kila la kheri katika biashara yako ya matofali
 

Mkuu, hamidu mahmoud, ulifanikiwa?
 
Kwa wastani baada ya kutoa gharama zote faida kwa kila tofali unalouza ni sh ngapi?
 
Habari zenu wadau,


Naomba kujua viability ya biashara ya kufyatua na kuuza matofali. Gharama za uwekezaji, gharama za uendeshaji na Faida au income ninayoweza kupata angalau kwa mwezi.

Msaada wenu wadau tafadhali.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Faida ipo kwani tunafyetua tofali 50 kwa mfuko badala ya 30 then tunapa maji mengi sana
 

Safi, ila point namba 4.
Lori kadhaa za mchanga au mchanga lori kadhaa.

Usihofu, ni kiswahili huyo.
 
wazo safi utapiga ela usirudi nyuma mzee tofali ziwe tu na viwango utakubali mwenyewe
 
Bei ya manual shingapi mkuu; Za umeme izo as we grow tutazinunua baadae!!! Alafu na Tani mmoja ya cement pale wazo inaweza ikawa inasimama kwa ngapi?
 
Mkuu nahitahi kidogo unifafanulie kuhusu malipo wanayostahili kulipwa vibarua kulingana na mfuko wa cement..ndio inakuwaje???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…