Ushauri: Biashara ya zoo, mtaji na eneo

Ushauri: Biashara ya zoo, mtaji na eneo

livescore

Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
93
Reaction score
40
Wakubwa shikamoo,wadogo hamjambo,

Wana jamvi, Naomba msaada kwa mtu anayefahamu,anayefanya biashara hii,wataalamu wa wanyama pori au wazo lolote na ushauri kuhusu wazo langu naomba anisaidie.

Huwa nawaza na kuona fursa ya kufanya biashara ya zoo,yaani mahali ninapoweza kuweka wanyama mbalimbali watu wakapita kuwaona,kupiga picha na kutoa kiingilio,

Lakini sifahamu sheria za wanyama pori,usajiri wa biashara hiyo,na namna ya kuiendesha na mtaji kiasi gani unahitajika lakini pia namna ya kuwapata wanyama hawo mfano simba,chui na baadhi ya nyoka wa maonyesho.

Naomba msaada zaidi
 
Kuna uzi kama huu uliwahi kuandikwa humu kwa kina hembi search kwanza.

Lakini kama sikosei kwa muono wangu ili uweze ku manage biashara hii kwa kiwango cha kati si chini ya 150m - 200m
 
Kuhusu wanyama wala usijali kuna baadh ya watangazania wanaotaka kwenda jumba jeupe unaweza kuingia nao mkataba mana hawana tofauti sana na hao wanaopatikana serengeti,mikumi nk
 
Back
Top Bottom