Ushauri: Bondia Karim Mandonga achana na wazo la kugombea Ubunge, utalogwa uache magari yako uliyopewa zawadi

Ushauri: Bondia Karim Mandonga achana na wazo la kugombea Ubunge, utalogwa uache magari yako uliyopewa zawadi

uwe hodari

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2022
Posts
4,045
Reaction score
8,608
Nimepata taarfa bondia namba moja Afrika Mashariki, Karim Mandonga anajipanga kunyakua jimbo la Morogoro Mjini

Ni kweli anaushawishi wa kushinda Ubunge kwasababu vijana wengi Tanzania wanampenda Mandonga ila sio rahisi kumwangusha Abood. Yule mzee ni anapiga vibuyu hatari km huamini uliza wataalamu wa jadi wanaomfanyia kazi

Ushauri wangu chukua form ya kugombea ubunge kupitia CCM atakufuata uvune mipesa ili ujitoe usikatae

Ila usigombee ubunge watakuibia tu hutapata
 
Kuna haja ije sheria ya ukomo wa ubunge. Kama vipi ukomo iwe awamu mbili tu ambapo ukiongoza ya kwanza unakaa kwanza pembeni ndo unapata tena sifa ya kuja kutafuta nafasi ya kumalizia awamu ya pili. Watu wapo wengi wanataka kuongoza lakini kuna watu wameng'ang'ania majimbo kama ya kwao
 
Atakuwa na tamaa

Hayo magari akabidhi huku 🤣🤣🤣
 
Walio kwenye Siasa mbona ni kama Mandonga tuu mdomo ndio mtaji akipigana huko baadae akagombele akale keki ya Taifa kila kikao 300,000 Tsh kama Mh Ndugai alikua Subwoofer hao wabunge wake wapoje wacha atumie fursa hizo wanamziki wameingia huko wengi kwa sababu ya Umaarufu,ukiutumia umaarufu vizuri utamsaidia....
 
Kuna haja ije sheria ya ukomo wa ubunge. Kama vipi ukomo iwe awamu mbili tu ambapo ukiongoza ya kwanza unakaa kwanza pembeni ndo unapata tena sifa ya kuja kutafuta nafasi ya kumalizia awamu ya pili. Watu wapo wengi wanataka kuongoza lakini kuna watu wameng'ang'ania majimbo kama ya kwao
Kwani kama unavigezo zaidi ya kiongozi aliyeyopo madarakani hujakatwazwa kugombea
 
Back
Top Bottom