USHAURI: Busara itumike kumsaidia kiafya msemaji wa Simba(Haji Manara).

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Kuna vipande vya video vinasambaa mtandaoni vikimuonyesha msemaji wa Simba Haji Manara akiwa jukwaani uwanjani wakati Simba ikicheza(Sina uhakika kama ni kule DRC dhidi ya AS Vita Club) huku akionekana anagugumia kwa maumivu kifuani huku akishika kifua kwa upande wa kushoto, akihema kwa shida baadaye akionekana akiwa hana utulivu na kukosa amani na furaha. Baadhi ya wataalamu wa afya wanasema huenda Haji Manara alipatwa na shambulizi la moyo kutokana na msongo mkubwa wa mawazo(Over stress) au taharuki ya kupitiliza(Panic attack) kiasi cha kupelekea yote hayo. Na moja ya mapendekezo yao ni kuhakikisha Simba inampeleka kwa wataalamu wa Afya wa moyo ili kumchunguza zaidi na pia ikiwezekana kumpumzisha na mambo ya soka kwa sasa(kama sio maisha yake yote) ili mwili upate namna ya kuhimili na kurejea sawa na vile vile kuepusha kujirudia tena kwa kitu hicho cha hatari ambacho kitabia kina mtindo wa kujirudiarudia na kuhatarisha maisha ya mtu.

ANGALIZO.
Jambo hili limetwa humu kwa misingi ya Kitaalamu na kiutu, na wala sio kiushabiki. Maoni yetu yajikite hapo.
 
Huyo ni mropokaji na sio msemaji...

Sijui kwanini kazi hizi za wasemaji zinapewa watu wasio na staha, kunena ovyo, wasio na elim nk...

Embu wajifunze kwa clubs kubwa duniani wasemaji wanavyokuwa smart sana.

Kwanza kwa wenzetu wasemaji wa Timu ni Makocha sio kama huku kwetu kwa Waganga njaa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
👊👊👊 Hahahahaha. 5. THIS IS SIMBA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…