Ushauri: Bustani ya Miti ya Matunda katika Nyumba

Ushauri: Bustani ya Miti ya Matunda katika Nyumba

n
Asante kaka kwa ushauri,Ubarikiwe.
Michikichi
nimeweka kama attraction ya viota vya ndege na ndege wenyewe pia ili kuwe na mvuto kwa aina nyingi za ndege,naweza kuipunguza ikawa 2.
Apples,
nitaziondoa kwenye list kwa ushari wako
Mishokishoki -
Nitapitia Kizimbani kupata ushauri wa kitaalam,na nitaongeza kuwa mitatu kwa ushauri wako
Mangosteen
Ubarikiwe nimeongeza kwenye list,na pia nitapitia Kizimbani kwa ushauri
Miembe:
Hii ni ya Kisasa
Mitufaa(Malay Apple)
Ubarikiwe kwa ushauri,maana mie nipo huku fuoni Zanzibar,ipo kibaoo na inakivuli kizui kweli,maana majani yake mapana kama Mshokishoki.
Nimeongeza kwenye list
Minazi:
Nitachukua kitamli ndio plan yangu,maana lengi ni kwa madafu na sio nazi za kupikia,asante kwa msisitizo
mzambarau, mkunazi au mkwaju
Hii nayo changamoto,nimeliona hili,nita edit lits yangu
Maana sidhani kama kuna mizambarau au mikwaju ya kisasa,yoote nikiona ni mikubwa saana.

Kuhusu kuwa na eneo la mboga mbona ipo considered kaka,ni muhim pia sana

Kuhusu Spacing:
Hili ndio muhim sana ili nijue nachukua akubwa gani,na ndio maana nasubiria list ya mazao itimie na ushauri wenu kama huo then niweze kupata zaidi uelewa wa spacing.
Maana ndio itafanya kupendeza kwa madhari husika[/QUOTE

Nimeshindwa kuchangia kwa mshangao na utamu wa somo. Kwangu hii ndiyo nadharia halisi ya Great Thinkers.Kuna kitu kikubwa mno ninajifunza.Nikushauri tu upande wa mchikichi kama lengo ni kuvutia ndege tu,kwa wingi huo wa aina tofauti za matunda utakuwa na ndege wa kila aina.Usisahau kuanza mapema kuchonga mizinga ya nyuki na kutafuta nyuki wasiouma.Usipoweka nyuki wasiouma watakuja hata bila kuwaita wanaouma,maana unatengeneza Eden ndogo nyumbani kwako.Hongera.
 
Hiyo ni idea nzuri. Mimi kwangu nimefanya hivyo, nimepanda aina nyingi ya miti ya matunda na sasa yana mwaka wa pili hivi. Mingine tayari imeanza kuzaa (mipapai, mipera, carambola).

Ila ningekushauri miti ifuatayo uwe na hadhari:
-Michikichi ni ya nini kwenye yard? Ikiwa utapenda labda panda mmoja au miwili tu.
-Apples haziwezi kuota kwenye joto, zinahitaji kipindi cha baridi katika ukuaji wake, sawasawa na peaches na plums (matunda damu)
-mishoki shoki hebu cheki nadhani unahitaji mitatu (ulizia kama iko dume na jike tafauti.... ni vyema ukaenda kituo cha utafiti kizimbani kupata usahihi zaidi). Pia upate aina ya 'nyama peke yake' - ulizia kwa wenye mishoki shoki aina hii maeneo ya Mwera.
-mangosteen (ulizia kizimbani) matunda yake ni safi sana.
-miembe panda ile midogo ya kisasa.
-mitufaa (malay apples) iko mekundu na meupe. Ni mizuri kuipanda karibu na nyumba
-minazi chukuwa kitamli (ya madafu) ndiyoo mizuri karibu na nyumba. Ile mirefu (east african tall) yana changamoto zake, kwani nazi ikidondoka kutoka juu ni hatari.
- mzambarau, mkunazi au mkwaju kwa nyumba ya kawaida inakuwa mikubwa sana, labda kama utakuwa na shamba.

Ingependeza zaidi ukiacha sehemu ndogo kwa ajili ya kupanda mazao ya bustani - mchicha, matembere, nyanya, pilipili na vyengine vya msimu

Kuhusu spacing kwa miti aina ya mifenesi, miparachichi unatakiwa angalau iwe mita 5 x 5, na itapendeza zaidi ikiwa utapanda kwa mistari.
Habar yako Mangosteen na Malayapple ntazipata wp kwa Dar karibu na maeneo ya kigamboni
 
Habari wakuu,
Hembu wazoefu wa kilimo,nipeni ushauri huu.

Kwanza angalizo la mwazo:-

Miti hiyo ni kama decoration,badala ya kuwa na mauwa kwenye Nyumba,nimeamua iwe ni Royal Fruits House of my dream.
Kwahiyo sio kwa biashara.Ni matumizi ya inhouse or just friend wataotembelea na pia neighbors .

Niliipenda hii maana niliikuta Kenya,kuna biz man mwenzangu yeye alijenga house ana courtyard kubwa kiasi alipanda fruits trees kwa mfumo mzuri sana.Na alipoimaliza na kuipangisha basi ananiambia Customers wengi walikuwa attracted na miti ya matunda,licha ya kwamba alikuwa na ziada ya Swimming pool na Tennis Court.So,alikuwa pesa tamu sana kwa wa Russia Waliokodi waliokuwa attracted na mfumo wa nyumba,na huyu jamaa alinipa Idea na kuniambia kwamba dunia inabadilika.
Na mfumo alioutumia ni kwamba alinunua kiwanja kisha akapanda miti,then after two years akaanza kujenga,so in 3 years miti yake ikawa imeanza ku bear fruits.

Naomba mnijuze sasa wazoefu.

Mie nimelist miti hii hapa chini,ningependa kujua kwanza kama hakuna miti yenye allergy na mwenzie(hahaha).

Najua swali linalofuata ni kujua ardhi,ufupi itakuwa Kigamboni au Chanika ndiko ambapo ninaplan kutia team January kuchukua eneo.
Pia nina plan kama ardhi haita suite baadhi ya mazao,niliona Kenya wanahamisha udongo na kuweka kwenye pot,au kuongezea chini ili ku suite zao husika,maana altitude inaonekana haina athari kubwa sana.

-Je mazao hayo yanaweza kuwa pamoja
-Kwa wazoefu,ni ukubwa gani wa eneo natakiwa niwe nao kwa miti yote hiyo.Just for trees tu,maana ukubwa wa House,swimming pool,tennis Court(converted to Basketball pitch and Volleyball pitch) ukubwa wake ninao tayari.

-Ushauri mwingine wa ziada pia unakaribishwa

List hapa chini ila mwenye ziada anaweza kuongeza

Aina ya mti na idadi yake

1)Miembe 2
2)Mipera 2
3)Avocado 1
4)Michungwa 2
5)Michenza 2
6)Ndimu(Lime) 2
7)Lemon 1
8)Komamanga 2
9)Shokishoki(Rambutan) 2 -3(Imependekezwa na mdau idadi iwe mitatu by bintikikongwe
10)Minazi 6 (Kitamli,kwa madafu tuu)
11)Michikichi 4 (Lengo ni kuvutia ndege na viota vyake)

12)Apples 6 (Hii imefelishwa moja kwa moja na wadau waliotangulia
13)Stafeli 3
14)Bilimbi(mbilimbi) 2
15)Topetope(Custard Fruit) 2
16)Carambola 2
17)Minanasi 10
Ziada nimeyopata kwa mdau humu Chaula Rich
Naongeza
18)Fenesi(Jack Fruit) 1
Ziada ya mdau chuma cha rel
19)Bungo Tree 2
20)Mipapai 6
Ziada ya mdau Rolandi
21: Pilipili,miti 10 au 20 ya aina tofauti

Ziada kwa mdau
Kingmairo
22:Zambarau 1 (umefelishwa na bintikikongwe kwa kuwa unachukua eneo kubwa sana unless kuwe na ya kisasa
23:Mangosteen 2 : (imependekezwa na Bintikikongwe)
24:Mitufaa (malay apples) 2: (imependekezwa na Bintikikongwe)


Miti tiba:
Karafuu 2
Mironge 2
Mkunazi 1
Update mkuu
 
Asante kaka
Lemon nimeweka kwenye list
Matunda damu,hapa naona kama kila mkoa wanaita matunda damu ila ukiyaona yanakuwa tofauti,ila najua ni aina ya berries lakini sijajua ni yapi mkuu.
Kuhusu Piches,hili zao zilijua kaka
Fenesi,hili nilikuwa nafikiria kuwemo kwenye list.Nimeliweka,asante sana
Machungwa3
 
Kiongozi Asante kwa mrejesho wako. Mm nimeipenda n ninaicopy kwenda nayo katika shamba langu lililoko BAGAMOYO,FUKAYOSI ambalo nami nina plan kama yako lakini kwngu nitaweka makazi baada y miaka 3 tu.makazi y kuenda siku z wkend na sikukuu kupumzika n ndugu n jamaa. Ni heka chache tu kama 2 hv. Nimesafisha moja heka kwnza kwajili y kitu kama hii.nimepata kuvutiwa n mawazo kama haya. Sasa ni Wakati wa vitendo. Eeh mungu naomba uwezeshe ndoto yangu hii kutimia. Amen.
HII NI SEHEMU YA SHAMBA LENYEWE.
a1c7b7a895b606e44ff4451f8a9d5981.jpg
37d81b146294658cd688d253824128b8.jpg

SEMA MM NITAONGEZA NA MBUZI WA KUZAA MAPACHA KAMA KITOWEO TU.
Ng'ombe wa Maziwa usisahau!
 
Nimshukurubaliyeanzisha huu Uzi, nilichukua hii idea na kuifanyia kazi mwaka 2016, kwasasa nyumbani kwangu Kuna matunda yafuatayo ambayo yameshaanza kuzaa Toka mwaka 2022
1. Mipera 2
2. Chungwa 3
3. Chenza 2
3. Miembe 6
4. Komamanga 4
5. Stakafeli 2
6. Zaituni 1
7. Parachichi 2
8. Papai 3
9. Tunda Damu 2
10. Passion 2
11. Kuna tunda lisijui jina 1
12. Pilipili 2
Nb. Niliongezea na miti 2 ya kivuli.
Kwa Sasa Nina matunda mengi nyumbani kwangu, tunatumia pamoja na familia bila kusahau majirani
 
Back
Top Bottom